

Lugha Nyingine
Mashirika ya Umoja wa Mataifa yaonya juu ya janga la njaa linaloikabili Somalia
MOGADISHU - Mashirika manne ya Umoja wa Mataifa Jumatatu wiki hii yameonya juu ya njaa kali inayokuja nchini Somalia huku hatari ya njaa ikiongezeka katikati ya misimu minne ya mvua bila mvua kunyesha katika historia.
Mashirika hayo yakiwemo Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (FAO), Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) kwa pamoja yametoa wito kwa wafadhili kuongeza misaada yao kwa haraka ili kuepusha njaa.
"Lazima tuchukue hatua mara moja ili kuzuia maafa ya kibinadamu. Maisha ya watu walio hatarini zaidi tayari yako hatarini kutokana na utapiamlo na njaa, na hatuwezi kusubiri tangazo la uwepo wa njaa ili tuchukue hatua," El-Khidir Daloum, Mkurugenzi wa WFP nchini Somalia amesema katika taarifa ya pamoja iliyotolewa mjini Mogadishu, Mji Mkuu wa Somalia.
Daloum amesema ni mbio dhidi ya wakati ili kuzuia njaa, akiongeza kuwa WFP inaongeza kadiri inavyowezekana, ikiweka kipaumbele cha rasilimali chache kuokoa wale walio katika hatari zaidi.
"Lakini kama takwimu hizi mpya zinavyoonyesha, kuna hitaji la dharura la rasilimali zaidi ili kukabiliana na janga hili la njaa linalozidi kuongezeka," amesema.
Mashirika hayo ya Umoja wa Mataifa yamesema misimu minne mfululizo ya mvua iliyokosa mvua, kupanda kwa bei, na upungufu wa misaada ya kibinadamu kumesababisha ongezeko la asilimia 160 la watu wanaokabiliwa na viwango vya ukosefu wa usalama wa chakula, njaa na magonjwa nchini Somalia.
Huku kukiwa hakuna kikomo kwa ukame mbaya unaoathiri nchi hiyo, mashirika hayo yameonya kwamba hatari ya njaa inakaribia zaidi kuliko hapo awali.
Adam Abdelmoula, Mratibu Mkazi na Misaada ya Kibinadamu amesema Somalia iko katika hatari ya kuingia misimu ya mvua mitano mfululizo inayokosa mvua ambayo haijawahi kushuhudiwa, akimaanisha mamia ya maelfu ya watu wanakabiliwa na hatari ya njaa.
"Tunatazama janga linaloweza kutokea; kushindwa kuchukua hatua sasa itakuwa janga kwa familia nyingi nchini Somalia," Abdelmoula amesema.
Amesema njaa iligharimu maisha ya Wasomali 260,000 Mwaka 2010-2011, akiongeza kuwa hii haiwezi kuruhusiwa kutokea tena Mwaka 2022.
"Ni dharura kwamba inabidi kufanya zaidi ili kuepusha hatari hii na kufanya sasa," afisa huyo wa Umoja wa Mataifa amesema.
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na washirika wenzi sasa wanaelekeza rasilimali zao chache katika kuzuia njaa ili kuwalinda watu walio hatarini zaidi nchini humo, huku mashirika ya hali ya hewa yakionya kuwa msimu mwingine wa mvua za kiwango cha chini ya wastani unaweza kufuata baadaye mwakani.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma