China yaongoza duniani kwa idadi ya hataza za teknolojia ya 5G zilizotangazwa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 08, 2022

BEIJING - China inamiliki karibu asilimia 40 ya hataza muhimu za kawaida za teknolojia ya 5G, ikibaki kileleni mwa viwango vya ubora duniani, kwa mujibu wa ripoti mpya ya Idara ya Taifa ya Hakimiliki ya Ubunifu ya China.

Ripoti hiyo ilisema kuwa, zaidi ya hataza muhimu 210,000 za 5G zilitangazwa kote duniani kwa sasa, zikihusisha karibu maeneo 47,000 ya hataza. China ilitangaza maeneo 18,728 yenye hataza, ikiwa ni sawa na asilimia 39.9 ya jumla ya ile ya duniani, ikifuatiwa na Marekani kwa asilimia 34.6 na Jamhuri ya Korea kwa asilimia 9.2.

Maeneo ya hataza ni mkusanyiko wa maombi ya hataza yanayojumuisha maudhui sawa au yanayofanana ya kiufundi.

Kampuni ya teknolojia ya China ya Huawei ilitangaza maeneo 6,583 ya hataza, ikiwa na asilimia 14 na kuchukua nafasi ya kwanza kati ya waombaji wa kimataifa.

Ripoti hiyo pia inaonyesha kuwa kati ya waombaji 15 wa juu wa hataza duniani, kampuni saba ni za China, na mbili kutoka kila nchi za Marekani, Japan, Ulaya na Jamhuri ya Korea.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha