Mateso ya kiholela katika "maeneo meusi" ya Marekani yanakiuka haki za binadamu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 08, 2022

Marekani kwa muda mrefu imekuwa ikijitangaza kama mtetezi wa haki za binadamu, lakini kile kinachojulikana kama vitendo vya haki za binadamu vya Marekani imethibitisha kuwa ni jani la mtini linalofunika matukio ya mara kwa mara ya mateso ya kiholela na kashfa za unyanyasaji wa wafungwa katika "maeneo meusi." 

Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) limeanzisha "maeneo meusi" katika nchi nyingi kwa kisingizio cha "Vita dhidi ya Ugaidi" ili kuwaweka kwa siri washukiwa wa ugaidi chini ya vizuizi holela na kuwatisha ili kukiri makosa kwa kutumia mbinu za mateso.

Gazeti la The Guardian la Uingereza liliripoti kwamba, kwa mujibu wa ripoti mpya ya Serikali ya Marekani iliyofichuliwa hivi karibuni, mfungwa katika kituo cha siri cha CIA nchini Afghanistan akiwa hai alitumiwa kama sampuli katika majaribio kuwafunza mbinu za kutesa wanafunzi wa masomo ya kuhoji washukiwa. “Mbinu zilizoimarishwa za kuwahoji washukiwa” ambazo ni kikatili na za kutisha, zikiwemo za mateso, kuoshwa na maji, kuwanyima usingizi, kugonga vichwa vya wafungwa kwenye kuta, na kumwagiwa maji baridi ya barafu, ambayo yote ni matendo ya kikatili dhidi ya ubinadamu, yameripotiwa kutumika katika hayo “maeneo meusi.”

Gharama ya mradi wa Vita iliyoandaliwa na Taasisi ya Watson ya Masuala ya Kimataifa na Umma katika Chuo Kikuu cha Brown iliyochapishwa mapema mwaka huu zilionyesha kwamba Marekani imetenga "maeneo meusi" katika angalau nchi na kanda 54 duniani kote, na imeweka kizuizini mamia kwa maelfu ya watu tangu mashambulizi ya 9/11, ikiwa ni pamoja na Waislamu, wanawake na vijana. Walipakodi wa Marekani wanatumia dola milioni 540 za kimarekani kwa mwaka kusaidia tu kuzuiliwa kwa wafungwa kwenye kambi ya kizuizini ya Ghuba ya Guantanamo.

Huku ikikanyaga utawala wa sheria na kukiuka haki za binadamu, Marekani aliyejipaka mafuta kuwa "nuru ya haki za binadamu", wakati huo huo imetoa mwanga wa kumulika wengine huku yenyewe ikijiweka gizani.

(Katuni na Ma Hongliang)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha