Hali ya wakimbizi na wahamiaji inasikitisha kwani ni vigumu kwao kuvuka mpaka wa Marekani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 09, 2022

(Katuni na Ma Hongliang)

Katika muda mrefu uliopita, Marekani ikijifanya kuwa mtetezi wa haki za binadamu ililaumu kila mara nchi nyingine kwa hali yao ya haki za binadamu, lakini kutokana na namna Marekani inavyowatendea wakimbizi na wahamiaji, hali ya uovu na unafiki wake imeonekana wazi.

Tangu mgogoro kati ya Russia na Ukraine ulipolipuka, Marekani ilitia moto kwa kuwasilisha silaha Ukraine, huku ikiahidi kupokea wakimbizi laki moja kutoka Ukraine. Lakini ikilinganishwa na mamilioni ya wakimbizi wa Ukraine waliolazimika kukimbia makazi yao, ahadi ya laki moja ya Marekani ni watu wachache sana. Hata hivyo, Marekani inaonekana kama haina nia ya kutimiza ahadi yake. Katika miwezi mitatu iliyopita, Marekani ilikubali maombi ya wakimbizi 12 tu wa Ukraine.

Ahadi ya Marekani ya “kupokea wakimbizi na kuheshimu haki za binadamu” ni maneno matupu tu. Kujenga ukuta kwenye mpaka wa Marekani na Mexico, watekelezaji wa sheria waliopanda farasi waliwafukuza wahamiaji, na kuwaweka kizuizini kiharamu watu wengi ndani ya vituo vyenye hali ngumu kwa muda mrefu, na kutekeleza kwa nguvu sera ya "kutenganisha wazazi wahamiaji na watoto wao"...... yote hayo yameonesha Marekani ndio mvamizi wa haki za binadamu za wakimbizi na wahamiaji.

Badala ya kutumia nguvu zake kuingilia kati nchi nyingine, bora Marekani ichunguze kwa umakini na kurekebisha uhalifu wake mwingi kuhusu suala la wakimbizi na wahamiaji.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha