

Lugha Nyingine
Botswana kufuatilia miradi ya nishati safi ili kutengeneza nafasi za kazi
Rais wa Botswana Mokgweetsi Masisi (wa nne kushoto), Waziri wa Mambo ya Nje Lemogang Kwape (wa tatu kulia) na wageni wengine wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa semina ya Botswana kuhusu uchambuzi wa baada ya Baraza la Uchumi Duniani (WEF) iliyofanyika mjini Gaborone, Botswana, Juni 8, 2022. Botswana imepanga mipango na miradi kadhaa katika sekta ya nishati safi, wakati nchi hiyo ya Kusini mwa Afrika inatafuta njia za kuhama kutoka kwenye uchumi unaotegemea rasilimali kwenda kwenye ule unaotegemea maarifa na kutengeneza nafasi za kazi. Rais Mokgweetsi Masisi ameweka bayana hili Jumatano wiki hii alipokuwa akitoa hotuba kuu kwenye semina hiyo ya uchambuzi wa baada ya Baraza la Uchumi Duniani (WEF) mjini Gaborone. (Picha na Tshekiso Tebalo/Xinhua)
GABORONE - Botswana inafuatilia mipango na miradi kadhaa katika sekta ya nishati safi, wakati nchi hiyo ya Kusini mwa Afrika inatafuta njia za kuhama kutoka kwenye uchumi unaotegemea rasilimali kwenda kwenye ule unaotegemea ujuzi na kutengeneza nafasi za kazi.
Rais wa nchi hiyo Mokgweetsi Masisi ameweka bayana hili Jumatano wiki hii alipokuwa akitoa hotuba kuu wakati wa semina ya Botswana kuhusu uchambuzi wa baada ya Baraza la Uchumi Duniani (WEF) mjini Gaborone.
"Katika azma yetu ya kuhama kutoka kwenye uchumi unaotegemea rasilimali na kwenda kwenye uchumi unaotegemea maarifa na kutengeneza ajira, kuna mipango na miradi kadhaa ambayo tunafuatilia, ambayo baadhi iko katika sekta ya nishati safi," amesema Masisi.
Ameongeza kuwa, Botswana, ambayo kwa sasa inapitia mpango wake wa rasilmali jumuishi ili kupanua mchango wa nishati inayotokana na jua kwenye mfumo wa nishati wa Botswana, inafanya jitihada kubwa ili kuhakikisha kuwa kuna ufadhili wa programu na miradi katika sekta ya nishati safi.
Kwa mujibu wa Masisi, upanuzi unaotarajiwa wa mchango wa nishati inayotokana na jua katika mfumo wa nishati wa nchi hiyo unatokana na mawio bora ya jua ya Botswana kwa nishati inayotokana na jua.
Mpho Regoeng, mtaalam wa kujitegemea wa nishati anayeishi Gaborone, Mji Mkuu wa Botswana, amesema kwenye semina hiyo kuwa uwekezaji wa kijani unasababisha mabadiliko ya kazi badala ya kusubiri kazi kwa muda mrefu na inaweza kutengeneza ajira mpya kwa muda mfupi ikiwa itatekelezwa katika uchumi.
Regoeng ametoa mfano kwa kusema kuwa kuwekeza katika nishati inayotokana na jua ya photovoltaic kunatengeneza wastani wa ajira mara 1.5 zaidi ya kuwekeza kiasi sawa cha fedha katika nishati inayotokana na mafuta.
Kwa mujibu wa Shirika la Kazi Duniani, kuhamia kwenye uchumi unaojali mazingira kunaweza kutengeneza nafasi mpya za kazi milioni 24 duniani kote ifikapo Mwaka 2030 ikiwa sera zinazofaa zitawekwa.
Rais wa Botswana Mokgweetsi Masisi akizungumza kwenye semina ya Botswana kuhusu uchambuzi wa baada ya Baraza la Uchumi Duniani (WEF) huko Gaborone, Botswana, Juni 8, 2022. (Picha na Tshekiso Tebalo/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma