Magereza ya Marekani yawa mashine ya kuchapisha noti ya kufanya biashara kwa kisingizio cha “haki”

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 10, 2022

(Katuni na Ma Hongliang)

Mfumo mkubwa wa magereza nchini Marekani unafanya biashara kwa kisingizio cha “haki”.

Mnamo mwaka 2019, mfumo wa mahakama wa Marekani uliwafunga watu milioni 2.1 hivi, na watu zaidi ya laki moja kati yao walifungwa ndani ya magereza ya kibinafsi. Kampuni zinazoendesha magereza zinasaini mkataba kwa kupitia serikali, huku serikali ikilipa malipo ya chini zaidi kwa magereza ya kibinafsi. Kwa kawaida malipo hayo yanategemea idadi ya wafungwa. Kwa hivyo ili kusaini mkataba, kila mwaka magereza ya kibinafsi yanashawishi wabunge wa taifa, na kutoa ufadhili wa kisiasa. Kampuni hizi hata zinatoa rushwa kwa maofisa wa mahakama ili kuongeza “ idadi ya wafungwa” magerezani. Maofisa mawili wa Jimbo la Pennsylvania waliwahi kupokea rushwa wakifunga vijana zaidi ya 4000 kwenye gereza la kibinafsi, na baadaye ilikuwa kashifa iliyojulikana ya “kubadilisha watoto kuwa fedha”.

Ili kupata faida kubwa zaidi, magereza ya kibinafsi hata yanawafanya wafungwa wafanye kazi kama watumwa. Wamiliki wa magereza ya kibinafsi wamechuma pesa nyingi sana. Kampuni mbili kubwa zaidi za magereza ya kibinafsi nchini Marekani zilipata mapato ya Dola za Marekani bilioni 1.9 na bilioni 2.3 kwa kila moja mwaka 2020.

Tukisema magereza ya kibinafsi ya Marekani yamekuwa mashine ya kuchapisha noti, basi damu na machozi ya wafungwa ni wino wake.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha