Uchumi wa China waonyesha kasi nzuri ya kufufuka Mwezi Mei

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 16, 2022

Mfanyakazi akibeba bidhaa katika kiwanda cha Shirika la SMC kilichopo Beijing kwenye Eneo la Maendeleo ya Kiuchumi na Kiteknolojia la Beijing, Juni 4, 2022. (Xinhua/Peng Ziyang)

BEIJING - Uchumi wa China umeshinda hatua kwa hatua athari za janga la UVIKO-19, huku viashiria vikuu vikionyesha kuimarika kwa kasi ndogo katika Mwezi Mei, Fu Linghui, Msemaji wa Idara ya Taifa ya Takwimu ya China, alisema Jumatano ya wiki hii.

"Uchumi unaonyesha kasi nzuri ya kufufuka," Fu amesema katika mkutano na waandishi wa habari, lakini alionya kuwa kuimarika kwa uchumi bado kunakabiliwa na matatizo na changamoto nyingi.

Uwekezaji wa mali zisizohamishika uliongezeka kwa asilimia 6.2 katika miezi mitano ya kwanza, ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 6.8 katika miezi minne ya kwanza.

Pato la viwanda liliongezeka kwa asilimia 0.7 Mwezi Mei kutoka mwaka uliopita baada ya kushuka kwa asilimia 2.9 Mwezi Aprili.

Mauzo ya bidhaa nje ya China yaliongezeka kwa asilimia 15.3 katika Mwezi wa Mei, ambayo ni ya kuvuka matarajio, huku viwanda vikianza tena uzalishaji na vikwazo vya usafirishaji kupungua.

Kiwango cha ukosefu wa ajira mijini kilichofanyiwa utafiti kilishuka hadi asilimia 5.9 Mwezi Mei kutoka asilimia 6.1 Mwezi Aprili.

Mauzo ya rejareja yalipungua kwa asilimia 6.7 Mwezi Mei, ikilinganishwa na yale ya wakati huo wa mwaka uliopita, na kupungua kwa asilimia 11.1 Mwezi Aprili.

"Ununuzi wa bidhaa bado unaimarika kutokana na janga la korona na utaendelea na kasi huku ajira zikisalia kuwa tulivu," Fu amesema.

"China inatarajiwa kurekodi ukuaji wa uchumi unaokubalika katika robo ya pili ikiwa janga la korona litadhibitiwa ipasavyo na hatua za kukuza uchumi zinaanza kutekelezwa," msemaji huyo amesema.

Alisema, kwa kutazama siku za baadaye, China itaratibu ipasavyo udhibiti wa janga la korona na maendeleo ya kiuchumi na kijamii, kuongeza kasi ya marekebisho ya sera za jumla, na kufanya kila juhudi kuhakikisha utekelezaji wa sera za ukuaji wa uchumi ili kukuza ufufukaji endelevu wa uchumi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha