

Lugha Nyingine
Ripoti yaonesha watumiaji wa malipo ya mtandaoni nchini China wafikia Milioni 900
Mhudumu wa kujitolea akiwasaidia wazee kutumia APP ya malipo ya mtandaoni kwenye moja ya makazi katika Eneo la Fengtai la Beijing, Mji Mkuu wa China, Novemba 12, 2021. (Xinhua/Li Xin)
BEIJING – Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa Jumatano wiki hii na Shirika la Malipo na Ushughulikiaji wa vifurushi vya bidhaa la China, idadi ya watumiaji wa malipo ya mtandaoni nchini China ilifikia milioni 904 mwishoni mwa Mwaka 2021.
Ripoti hiyo inasema, idadi hiyo ni sawa na asilimia 87.6 ya watumiaji wote wa mtandao wa intaneti nchini China na ni ongezeko la karibu watu milioni 50 kutoka mwaka mmoja uliopita.
Mwenendo wa China wa watu kutotumia fedha taslimu na kadi kwa ajili ya malipo unaendelea kukua, ukijumuisha idadi inayoongezeka ya mazingira ya kuanzia kuagiza chakula hadi kulipa nauli ya mabasi. Benki za China zilishughulikia miamala hiyo ya mitandaoni iliyofikia bilioni 102.28 ikiwa na thamani ya jumla ya yuan trilioni 2,353.96 (kama dola za kimarekani trilioni 350) mwaka jana, ikiwa ni mara 5.32 na mara 2.86 ya Mwaka 2012.
“Ushindani unapozidi kuongezeka, mkusanyiko wa soko wa sekta hiyo ulipungua mwaka jana”, Naibu Katibu mkuu wa shirika hilo, Wang Suzhen alisema.
Benki 10 bora zaidi katika malipo ya mtandaoni zilichangia asilimia 83.75 ya jumla ya kiasi cha malipo ya mtandaoni ya wanachama wa shirika hilo ambao ni wateja wa benki katika Mwaka 2021, ikiwa ni kiwango cha chini kwa asilimia 7.63 mwaka hadi mwaka, na mashirika 10 makubwa zaidi ya malipo hisa zao zilipungua kidogo kwa asilimia 0.48 hadi asilimia 96.25.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma