

Lugha Nyingine
Hospitali ya muda ya UVIKO-19 ya mwisho yafungwa Shanghai
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 16, 2022
Tarehe 15, Juni, Hospitali ya muda ya Kituo kipya cha Maonesho ya Kimataifa cha Shanghai kilifungwa. (Picha/Xinhua)
Hospitali ya muda ya mwisho ya Shanghai iliyotoa matibabu kwa wagonjwa wa korona katika wakati wa kutokea tena maambukizi ya virusi vya korona wa hivi karibuni ilifungwa Jumatano wiki hii.
Hospitali hii iko kwenye Kituo kipya cha Maonesho ya Kimataifa cha Shanghai, kilikuwa hospitali ya kwanza yenye uwezo wa kupokea wagonjwa zaidi ya 10,000 na iliyotumika jijini katika wakati wa maambukizi ya virusi vya korona.
Hospitali hiyo ya muda yenye vitanda 14,000 iliwahi kupokea wagonjwa 47,920 katika siku 77 zilizopita. Mgonjwa wa mwisho aliondoka Jumanne asubuhi.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma