Mkurugenzi wa eneo la Afrika la Shirika la Afya Duniani asema nchi 8 za Afrika zimeripoti watu waliothibitishwa kuambukizwa virusi vya Monkeypox

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 17, 2022

Mkurugenzi wa eneo la Afrika la Shirika la Afya Duniani Machidiso Muti, alisema katika mkutano na waandishi wa habari kwa njia ya mtandao wa intaneti huko Brazzaville, mji mkuu wa Kongo-Brazzaville tarehe 16, kwamba jumla ya nchi 8 za Afrika zimeripoti watu waliothibitishwa kuambukizwa virusi vya Monkeypox.

Muti alisema katika mkutano na waandishi wa habari kwamba Ghana na Morocco ziliripoti kwa mara ya kwanza watu waliothibtishwa kuambukizwa virusi vya Monkeypox siku za hivi karibuni, na watu watano waliripotiwa nchini Ghana na mmoja nchini Morocco. Aidha, Nigeria, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ,Jamhuri ya Afrika ya Kati, Benin, Cameroon na Kongo-Brazzaville pia zimeripoti watu walioambukizwa virusi vya Monkeypox ambapo Nigeria, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Jamhuri ya Afrika ya Kati ndio nchi zilizogunduliwa wagonjwa 36, 10 na 8 ambao ni wengi zaidi kuliko nchi nyingine.

Muti alisema Shirika la Afya la Duniani linazisaidia nchi za Afrika kuharakisha upimaji na upatikanaji wa chanjo dhidi ya virusi vya Monkeypox na vifaa vya matibabu. Lakini shirika hilo kwa sasa halipendekezi udungaji wa chanjo dhidi ya virusi vya Monkeypox kwa watu wengi. Muti alitoa wito kuwa pande zote zinatakiwa kuimarisha ushirikiano katika kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Monkeypox ili kuhakikisha upatikanaji wa haki wa chanjo dhidi ya virusi vya Monkeypox na vifaa vya matibabu.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha