

Lugha Nyingine
Ushirikiano wa chanjo kati ya China na Afrika Kusini chini ya mfumo wa utaratibu wa BRICS utanufaisha Afrika
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Numolux, Hilton Klein, ambayo ni mshirika wa Kampuni ya Sinovac ya China katika Afrika Kusini, alisema katika mahojiano maalum na waandishi wa habari wa Shirika la Habari la China, Xinhua hivi karibuni kwamba ushirikiano wa chanjo kati ya China na Afrika Kusini chini ya mfumo wa utaratibu wa BRICS siyo tu utaweza kuleta manufaa kwa afya ya watu wa Afrika, bali pia linaweza kusaidia Afrika kuongeza nafasi za ajira na kukuza uchumi wake, na hatimaye kuiwezesha "Afrika izalishe yenyewe chanjo zake".
Klein alisema kuwa Kampuni ya Numolux imeshirikiana na Kampuni ya Sinovac kufanya majaribio ya udungaji wa kipindi cha tatu wa chanjo dhidi ya virusi vya korona kwa watoto na vijana wenye umri wa miezi 6 hadi miaka 17 nchini Afrika Kusini kuanzia Septemba 2021.
"Majaribio yalionesha matokeo mazuri sana ambayo hakuna mmoja aliyepata athari mbaya. Matokeo ya takwimu yanaonesha kwamba idadi za vijana wanaolazwa hospitalini na waliokufa kwa sababu ya ugonjwa wa korona zimepunguzwa kwa kiasi kikubwa baada ya wao kudungwa chanjo ya Sinovac." Klein alisema.
Septemba 10, 2021, daktari akidunga dozi ya kwanza ya chanjo ya Sinovac kwa kijana aliyejitolea wa kwanza huko Pretoria, Afrika Kusini. Picha na Chen Cheng/Xinhua)
Chini ya mfumo wa utaratibu wa ushirikiano wa BRICS, China na Afrika Kusini zimefanya ushirikiano mbalimbali katika sekta ya chanjo dhidi ya virusi vya korona. Julai 2021, Mamlaka ya Usimamizi wa Bidhaa za Afya ya Afrika Kusini iliidhinisha matumizi ya dharura ya chanjo ya Sinovac dhidi ya virusi vya korona; Mwezi Februari mwaka huu, chanjo za Sinopharm ya China iliidhinishwa kwa matumizi rasmi nchini Afrika Kusini; Mwezi Machi mwaka huu, kituo cha utafiti na utengenezaji wa chanjo kilizinduliwa kwenye mtandao wa intaneti, kikiimarisha kwa kina ushirikiano katika nyanja za kufanya utafiti na majaribio pamoja, kushirikiana kujenga kiwanda na kutoa ruhusu kwa uzalishaji, na kinaonesha nchi za BRICS zimechukua hatua thabiti kwa kuimarisha ushirikiano katika sekta ya afya ya umma na utafiti na utengenezaji wa chanjo.
Klein alisema, " mbali na chanjo dhidi ya virusi vya korona, pia kuna chanjo za aina nyingine." Anaamini kuwa chini ya mfumo wa utaratibu wa ushirikiano wa BRICS, China na Afrika Kusini zitakuwa na ushirikiano zaidi katika sekta ya chanjo.
“Kwa kupitia mawasiliano na ushirikiano katika kujenga viwanda vya chanjo barani Afrika, watu wa Afrika siyo tu wanaweza kuboresha hali yao ya afya, lakini pia watapata fursa nyingi za ajira.” Alisema, wakati huo huo, bara la Afrika pia linaweza kuboresha uwezo wake wa kutengeneza chanjo chini ya uungaji mkono wa utaratibu wa ushirikiano wa BRICS, na kuwezesha chanjo zinazotengenezwa na bara hilo zinufaishe bara lake lenyewe."
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma