Kampuni 260 zinazoongoza sekta husika zathibitishwa kushiriki kwenye Maonesho ya 5 ya Uagizaji wa Bidhaa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 22, 2022

Picha ikionesha mkutano wa kutoa ripoti kuhusu hali ya maandalizi ya Maonesho ya 5 ya Uagizaji wa Bidhaa ya Kimataifa na hafla ya kutia saini tarehe 21, Juni. (Picha inatoka Xinhua)

Kamati ya maandalizi ya Maonesho ya 5 ya China ya Uagizaji wa Bidhaa ya Kimataifa (CIIE) Jumanne wiki hii ilisema, kwa jumla kuna kampuni 260 kati ya kampuni 500 bora duniani au zinazoongoza sekta husika zimethibitishwa kushirika kwenye Maonesho ya 5 ya China ya Uagizaji wa Bidhaa ya Kimataifa.

Naibu mkurugenzi wa maonesho hayo Sun Haicheng kwenye mkutano na waandishi wa habari alisema, kazi ya maandalizi ya maonesho hayo inaendelea vizuri, na maonesho hayo yatafanyika kuanzia tarehe 5 hadi 10, Mei huko Shanghai.

Bw. Sun alisema, ripoti kuhusu ufunguaji mlango duniani 2022 na kiwango cha ufunguaji mlango duniani vitatangazwa kwenye Baraza la Uchumi la Kimataifa la Hongqiao, ambalo ni shughuli itakayofanyika pamoja na Maonesho ya Uagizaji wa Bidhaa ya Kimataifa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha