Ofisa wa Zambia ashukuru makampuni ya China kwa kuisaidia Zambia kuwaandaa wataalam wa teknolojia ya mawasiliano ya habari

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 22, 2022

Tarehe 20, Waziri wa Elimu wa Zambia, Bw. Sia Kalima, alitoa shukrani zake kwa Kampuni ya Huawei na makampuni mengine ya teknolojia ya China kwa kutoa mafunzo kuisaidia Zambia kuwaandaa wataalam wa teknolojia ya upashanaji habari na mawasiliano ya habari.

Bw. Sia Kalima alisema kwenye hafla ya kuanzishwa kwa shughuli ya mafunzo ya “mbegu wa siku za baadaye” ya Kampuni ya Huawei kuwa, shughuli hiyo ya mafunzo itawasaidia wanafunzi wa Zambia kuongeza uwezo wao wa kupata nafasi za ajira, na kusaidia uvumbuzi wa kiteknolojia na maendeleo ya uchumi ya Zambia kwa kuwaandaa wataalam wa teknolojia ya mawasiliano ya habari nchini Zambia. Makampuni ya China kama Huawei yameweka mfano mzuri wa ushirikiano wa kusaidia Zambia na makampuni ya nchi hiyo kuwaandaa wataalam wa teknolojia ya mawasiliano ya habari, na kuunga mkono kwa nguvu maendeleo ya sekta ya teknolojia ya mawasiliano ya habari ya Zambia.

Konsela wa uchumi na biashara wa ubalozi wa China nchini Zambia Liu Guoyu alisema kuwa serikali ya China inayatia moyo makampuni ya China yatoe misaada kwa maendeleo endelevu ya pande zote ya Zambia ili kusukuma mbele kwa pamoja urafiki na ushirikiano kati ya nchi hizi mbili.

Mkurugenzi wa Ofisi ya Kampuni ya Huawei ya Usimamizi wa mambo ya nchi nyingi iliyoko nchini Afrika Kusini Bw.Li Fei, alijulisha kuwa tangu Mwaka 2015, Kampuni ya Huawei imefanya shughuli ya kutoa mafunzo ya "mbegu za siku za baadaye" nchini Zambia kwa miaka minane mfululizo. Wanafunzi hodari 30 wa vyuo vikuu vya sehemu mbalimbali za Zambia watashiriki kwenye shughuli hiyo ya mwaka huu. Watasoma somo la upashanaji habari na mawasiliano ya habari kwa njia ya video pamoja na wanafunzi wa vyuo vikuu wa nchi na kanda nyingine katika mafunzo ya wiki moja, na kufahamishwa utamaduni wa China.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha