Xi aendelea kuhimiza ushirikiano wa BRICS

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 22, 2022

Picha iliyopigwa Juni 17, 2022 kutoka angani ikionyesha jengo la makao makuu ya Benki Mpya ya Maendeleo (NDB), inayojulikana pia kama Benki ya BRICS, huko Shanghai, Mashariki mwa China. (Xinhua/Fang Zhe)

BEIJING –Rais wa China Xi Jinping atakuwa mwenyeji wa Mkutano wa 14 wa Wakuu wa nchi zinazounda Ushirikiano wa BRICS na Mazungumzo ya Ngazi ya Juu kuhusu Maendeleo ya Dunia, na kuhudhuria kwa njia ya video kwenye ufunguzi wa Baraza la biashara la BRICS siku ya baadaye wiki hii.

Mfumo wa BRICS unahusisha ushirikiano wa nchi tano kubwa zinazoinukia kiuchumi, ambazo ni Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini. Tangu ulipoanzishwa zaidi ya muongo mmoja uliopita, nchi za BRICS zimepata matokeo mazuri katika ushirikiano kwenye sekta za uchumi, biashara, siasa, usalama, uvumbuzi wa kiteknolojia, na pia mabadilishano ya kitamaduni na baina ya watu.

Kwa miaka mingi, Rais Xi amechangia ufahamu wake kwenye mfumo huo, na kuhimiza maendeleo ya jukwaa hilo la kimataifa la ushirikiano wa pande nyingi. Yafuatayo ni baadhi ya mambo muhimu ya nukuu zake kuhusiana na hili.

Kuhusu ushirikiano wa kiusalama na kisiasa

"Tuko katika kipindi kikubwa cha maendeleo, mabadiliko na marekebisho. Ingawa migogoro na umaskini bado havijaondolewa duniani, mwelekeo wa amani na maendeleo umeongezeka zaidi," Xi alisema kwenye ufunguzi wa Baraza la biashara la BRICS Septemba 3, 2017.

" Dunia yetu ya hivi leo inabadilika kuwa na ncha nyingi; utandawazi wa uchumi; uanuwai wa utamaduni; na jamii ya kidigitali. Sheria ya msituni ambapo wenye nguvu huwinda wanyonge na mchezo wa kutiana hasara vinakataliwa, na amani, maendeleo na ushirikiano wa kunufaishana umekuwa matarajio ya pamoja ya watu wote," alisema.

Picha iliyopigwa Tarehe 8 Desemba 2020 ikionyesha hafla ya uzinduzi wa kituo cha uvumbuzi cha BRICS cha uhusiano wa wenzi wa Mapinduzi Mapya ya Viwanda huko Xiamen, Mkoa wa Fujian, Kusini-Mashariki mwa China. (Xinhua/Lin Shanchuan)

Kuhusu Uchumi wa Dunia

"Tunapaswa kuhimiza ujenzi wa uchumi wazi wa kimataifa, kuendeleza biashara huria na kuwezesha uwekezaji, kujenga kwa pamoja minyororo mipya ya thamani ya kimataifa, na kusawazisha utandawazi wa uchumi," Xi alisema kwenye ufunguzi wa Baraza la biashara la BRICS Mwaka 2017, akibainisha: " Kufanya hivyo kutaleta manufaa kwa watu wa duniani kote."

"Tunahitaji kuunga mkono jukumu la Umoja wa Mataifa la kuratibu na kuhimiza ushirikiano wa maendeleo wa kimataifa ambao ni wenye usawa na uwiano, ili matunda ya maendeleo yasambae katika nchi zinazoendelea zaidi na mahitaji ya makundi ya watu maskini yatashughulikiwa vyema," alisisitiza pia.

Mwanamke akitazama picha kwenye Maonyesho ya tatu ya Pamoja ya Picha ya BRICS Media mjini Sao Paulo, Brazili, Oktoba 30, 2019. (Xinhua/Xin Yuewei)

Kuhusu mabadilishano kati ya watu

"Ushirikiano wenye mafanikio wa nchi za BRICS unathibitisha kwamba mifumo tofauti ya kijamii inaweza kubeba kila mmoja, kwamba mifumo tofauti ya maendeleo inaweza kufanya kazi na kwamba maadili tofauti yanaweza kutegemea nguvu ya kila mmoja. Tunapaswa kuwa wazi na shirikishi ili kujifunza kutoka kwa kila mmoja na kufanya maendeleo pamoja kwa kutafuta maelewano huku tukiweka kando tofauti," Xi alisema kwenye Mkutano wa Saba wa BRICS Julai 9, 2015.

"Sisi nchi za BRICS tunajivunia ustaarabu mkubwa. Linapokuja suala la kubadilishana kitamaduni na kati ya watu na watu, kuna mengi tunaweza kufanya pamoja," Xi alisema kwenye Mkutano wa Viongozi Wakuu wa nchi za BRICS huko Johannesburg, Afrika Kusini Julai 26, 2018. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha