Afrika Kusini yatarajia kunufaika zaidi kutokana na ushirikiano wa nchi za BRICS

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 23, 2022

Juni 10, Rais wa Afrika Kusini akijibu maswali kuhusu uhusiano wa kiwenzi mjini Cape Town, Afrika Kusini, Juni 10. (Picha na XINHUA)

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alisisitiza fursa zinazoletwa na kuimarishwa kwa ushirikiano akisema kuwa Afrika Kusini imenufaika kutokana na ongezoko la biashara na nchi nyingine za BRICS na juhudi za kupambana pamoja na maambukizi ya virusi vya korona.

Rais Ramaphosa na viongozi wa Brazil, Russia, India na China leo Alhamisi wamehudhuria kwa pamoja kwenye Mkutano wa 14 wa BRICS unaoandaliwa na China.

Katika taarifa yake iliyotolewa Jumatatu wiki hii, alisema nchi hizo tano zimetambua uhusiano wa wenzi wa kiuchumi wa nchi za BRICS, ambao unasaidia kuongeza ruhusa za kuingia kwenye soko, huku ukihimiza upanuaji zaidi wa maslahi ya nchi hizo katika biashara na uwekezaji kati yao uwe sehemu moja ya mazingira ya kirafiki ya shughuli zote za biashara.

Nchi za BRICS zimekuwa washirika wenzi muhumi zaidi siku hadi siku kwa Afrika Kusini. Ramaphosa alisema mwaka jana, uagizaji wa bidhaa kutoka nchi nyingine nne ulichukua asilimia 29 ya uagizaji wa bidhaa wa Afrika Kusini, huku mauzo ya nje kwao yakifikia asilimia 17 ya jumla ya Afrika Kusini. Aliongeza kuwa thamani ya biashara ya Afrika Kusini kwenye mfumo wa BRICS iliongezeka kwa dola za kimarekani bilioni 44 mwaka jana kutoka dola za kimarekani bilioni 30 hivi ya mwaka 2017.

Juni 1, kazi ya kuunda friji za Hisense ikifanyika huko Cape Town. (Picha na XINHUA)

Ramaphosa alisema kuwa nchi moja ya BRICS kutasaidia nchi hiyo kuongeza zaidi nguvu ya ushindani, mshikamano wa biashara na ongezeko la uchumi.

Alisema kuwa Afrika Kusini inanufaika kutokana na mfumo wa ushirikiano chini ya mfumo wa nchi za BRICS na imepata msaada wa dola za kimarakeni bilioni 5.4 kutoka kwa Benki ya Maendeleo Mapya iliyoazishwa na mfumo wa nchi za BRICS.

Ushirikiano mpana zaidi

Ramaphosa alisema kuwa Kituo cha Utafiti na Utengenezaji wa Chanjo cha nchi za BRICS, kilichoanzishwa Mwezi Machi mwaka huu kikilenga kuboresha uwezo wa kukabiliana na matukio ya dharura ya kiafya, ikiwa ni pamoja na kujiandaa kwa kukabiliana na maradhi ya kuambukiza ya siku za baadaye ambacho kitasaidia kuongeza uwezo wa utengenezaji wa chanjo wa Afrika Kusini na kanda nyingine za Afrika.

Mwezi huu, Mawaziri wa Kilimo wa nchi za BRICS walipitisha “Mkakati wa Ushirikiano wa Usalama wa Chakula wa nchi za BRICS”. Ramaphosa alisema pendekezo hili litaboresha uzalishaji wa kilimo kwa kupitia kuhakikisha nchi mbalimbali zinapata kwa urahisi zaidi utoaji wa mbegu, mbolea na pembejeo nyingine za kilimo.

Ramaphosa alieleza kuwa mkutano huo utajadili mageuzi ya mfumo wa pande nyingi ukiwemo Umoja wa Mataifa na juhudi za kuhimiza ongezeko endelevu, la haki na shirikishi la uchumi. Aliongeza kuwa mkutano wa viongozi utajadili namna ya kujenga dunia bora zaidi. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha