Mtaalam wa India asema mfumo wa BRICS unaziwezesha nchi zinazoendelea kueleza ufuatiliaji na matarajio

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 23, 2022

Picha iliyopigwa Septemba 8, 2021 ikionyesha miundo ya ndege wakati wa maonyesho ya BRICS kuhusu Mapinduzi Mapya ya Viwanda yaliyofanyika Xiamen, Mkoa wa Fujian, Kusini-Mashariki mwa China. (Xinhua/Lin Shanchuan)

NEW DELHI – Mtaalamu kutoka India amesema kuwa, mfumo wa BRICS unatoa jukwaa kwa nchi zinazoendelea kueleza ufuatiliaji wao na matarajio yao.

Mwenyekiti wa zamani wa Taasisi ya Utafiti ya Waangalizi wa jumuiya ya washauri mabingwa ya Mumbai, Bw. Sudheendra Kulkarni amesema katika mahojiano ya hivi karibuni na Shirika la Habari la China, Xinhua kwamba, mazungumzo ya ushirikiano wa pande nyingi kwenye Mkutano wa kilele wa BRICS unaofanyika sasa utakuwa tukio muhimu katika Mwaka 2022.

"Kuhusu mustakabali wa BRICS, viongozi wa nchi za BRICS wanapaswa kuzingatia kwa dhati jinsi ya kuifanya iwe na ufanisi zaidi," amesema.

Kwa kuzingatia kuongezeka kwa umuhimu wa kiuchumi na kisiasa wa masoko kadhaa mapya yanayoibuka na nchi zinazoendelea katika mazingira ya Dunia yanayobadilika kwa kasi, Kulkarni amesema uwezo wa BRICS wa kuchangia lengo la amani ya kikanda na Dunia hauwezi kupuuzwa.

Kuyajumuisha haya katika mfumo wa BRICS kutafanya jukwaa hilo kuwa lenye "uwakilishi zaidi," ameongeza.

"Mawazo yaliyowasilishwa na China, ambayo ni Pendekezo la Maendeleo ya Dunia, Pendekekezo la Usalama wa Dunia ... ni yenye manufaa makubwa kwa jumuiya ya kimataifa," amesema.

Huku kukiwa na mabadiliko ya hivi sasa ya mazingira ya kimataifa na janga la UVIKO-19, Kulkarni amesema nchi za BRICS lazima zipitishe mpango unaozingatia hatua ili kuleta utulivu wa hali ya uchumi wa Dunia, kuharakisha ufufukaji wa uchumi wa Dunia, na kurudisha kwa nguvu ajenda ya maendeleo yenye usawa kwenye siasa za kimataifa.

Amesisitiza kuwa, wakati mgogoro kiasili ni wa kimataifa, mwitikio wake pia unapaswa kuwa katika mfumo wa ushirikiano wa kimataifa.

“Hatua ya umoja ya nchi za BRICS na mataifa mengine yenye uchumi unaoibuka kwa hakika inaweza kusaidia ufufukaji wa uchumi wa Dunia baada ya kuathiriwa na mdororo unaohusiana na UVIKO-19,” Kulkarni amesema.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha