Rais Xi Jinping ahimiza nchi za BRICS ziwe na mshikamano, uwazi, amani na maendeleo

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 23, 2022

Rais wa China Xi Jinping akitoa hotuba kupitia njia ya mfumo pepe kwenye ufunguzi wa Baraza la Viwanda na Biashara la BRICS, Juni 22, 2022. (Xinhua/Ju Peng)

Rais wa China Xi Jinping Jumatano wiki hii alihudhuria ufunguzi wa mkutano wa Baraza la Viwanda na Biashara la BRICS na kutoa hotuba kwa njia ya video mjini Beijing, akizitaka nchi za BRICS kukumbatia mshikamano na kupanua ushirikiano wa kunufaishana na kufungua milango zaidi katika harakati za kutafuta amani, utulivu na maendeleo endelevu ya kimataifa.

"Mwelekeo wa kihistoria wa kufungua milango na maendeleo hautabadilika, na matumaini yetu ya pamoja ya kukabiliana na changamoto kwa ushirikiano yatabaki kuwa na nguvu kama zamani," Xi amesema, akitoa wito kwa nchi za BRICS kuzishinda changamoto na kusonga mbele kwa kufikia lengo la kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.

Mfumo wa BRICS unaoshirikisha nchi tano za Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini umepitia njia ya kung’ara katika miaka 16 iliyopita tangu kuanzishwa kwake Mwaka 2006, na umekuwa nguvu ya hamasa, imara na ya kiujenzi katika jumuiya ya kimataifa.

Mshikamano kwa amani, utulivu

"Tunapaswa kuwa na mshikamano na ushirikiano, kudumisha kwa pamoja amani na utulivu wa Dunia," Xi amesema, na kuongeza kuwa, amani, ambayo ni lengo la pamoja la binadamu, inapaswa kufuatwa na kulindwa na wote. Ametoa wito kwa nchi zote kuendelea kuwa wakweli katika kushikilia Mkataba wa Umoja wa Mataifa na kutimiza dhamira ya kudumisha amani.

Huku akisisitiza mapendekezo ya China ya Usalama wa Dunia na Maendeleo ya Dunia, amesema maafa ya siku za nyuma yanatuambia kwamba umwamba, siasa za makundi na makabiliano ya kambi hayaleti amani wala usalama, bali yatasababisha tu vita na migogoro. "Mgogoro wa Ukraine ni kengele nyingine ya kuamsha watu wote duniani. Unatukumbusha kuwa imani potofu katika kile kinachoitwa 'nafasi ya nguvu' na majaribio ya kupanua ushirikiano wa kijeshi na kutafuta usalama binafsi kwa gharama ya nchi nyingine itakuwa tu kujiingiza kwenye mtanziko wa kiusalama."

Ushirikiano kwa Maendeleo Endelevu

Maendeleo yana ufunguo wa kutatua matatizo mbalimbali magumu na kuleta maisha bora kwa wananchi. Katika hotuba hiyo, Xi ameeleza kwamba, kwa wakati huu, mchakato wa maendeleo duniani umegonga mwamba, na juhudi za kimataifa za kutekeleza Ajenda ya Umoja wa Mataifa ya Mwaka 2030 ya Maendeleo Endelevu zimepata vizuizi vikubwa.

Mjadala wa jopo wenye mada "Kuongeza kasi ya kubadilisha muundo wa uchumi bila kuchafua mazingira na kuhimiza maendeleo endelevu ya dunia nzima " ukifanyika wakati wa Baraza la Viwanda na Biashara la BRICS Beijing, Mji Mkuu wa China, Juni 22, 2022. (Xinhua/Yin Gang)

Ametoa wito kwa nchi za BRICS kuimarisha ushirikiano ili kulinda vyema usalama wa chakula na nishati, kutumia fursa zinazotolewa na mapinduzi mapya ya sayansi na teknolojia na mabadiliko ya viwanda, kusaidia nchi zinazoendelea kuharakisha maendeleo ya uchumi wa kidigitali na mabadiliko ya kijani, na kushiriki katika ushirikiano kwenye mapambano dhidi ya UVIKO-19 ili kuvishinda virusi mapema.

Kuweka uchumi wa Dunia wazi

Kwa sasa baadhi ya minyororo muhimu ya viwanda na ugavi inakabiliwa na usumbufu wa kimakusudi, bei za bidhaa zimepandishwa juu na zinabadilikabadilika, mfumuko wa bei duniani unaendelea kupanda, soko la fedha la kimataifa liko katika msukosuko, na kuimarika kwa uchumi wa Dunia kunazidi kuzorota.

Katika wakati huu muhimu, Rais Xi akisisitiza nafasi ya Shirika la Biashara duniani (WTO) na kutoa wito kwa nchi zote duniani kuimarisha uratibu wa sera za uchumi mkuu ili kuzuia kudorora na hata kuathiri kufufuka kwa uchumi wa Dunia, kuendelea kujitolea katika kufungua milango na kufanya ushirikiano , kuondoa vizuizi vyote kwa maendeleo yenye tija, na kuelekeza utandawazi katika mwelekeo wa haki. 

Mjadala wa jopo wenye mada ya "Kukumbatia uchumi wa kidijitali na kuhimiza ushirikiano wa wenzi wa BRICS kwa Mapinduzi Mapya ya Viwanda" ukifanyika wakati wa Baraza la Viwanda na Biashara la BRICS hapa Beijing, Juni 22, 2022. (Xinhua/Yin Gang)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha