WHO yasema mlipuko wa virusi vya Monkeypox sio “tukio la dharura la afya ya umma linalofuatiliwa duniani”

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 27, 2022

Shirika la habari la Reuters lilitoa habari zikisema kuwa Tarehe 25 kwa saa za huko, Shirika la Afya Duniani(WHO) lilisema kuwa maambukizi ya virusi vya Monkeypox hayajakuwa “ tukio la dharura la afya ya umma la dunia ”. Wakati huo huo Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dk. Tedros Adhanom Ghebreyesus alisema kuwa anaona wasiwasi sana juu ya maambukizi ya virusi hivyo.

Juni 24 kwa saa za huko, Serikali ya Mji wa New York ilifungua kliniki ya muda huko Manhattan ili kutoa chanjo dhidi ya virusi vya Monkeypox kwa watu ambao ni rahisi kwao kuambukizwa virusi. Picha hii ikionesha watu wakiuliza mambo kuhusu udungaji wa chanjo dhidi ya virusi vya Monkeypox. (Picha na Liao Pan/Chinanews)

WHO lilitoa taarifa kuwa ingawa kulikuwa na maoni tofauti ndani ya kamati yake, lakini hatimaye waliona kwa kauli moja kwamba katika kipindi cha hivi sasa, maambukizi ya virusi vya Monkeypox hayajakuwa “tukio la dharura la afya ya umma linayofuatiliwa na jumuiya ya kimataifa”.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dk. Tedros Adhanom Ghebreyesus alisema kwenye taarifa nyingine kuwa anaona wasiwasi mkubwa juu ya maambukizi ya virusi hivyo, alisema “ni dhahiri kuwa, hili ni tishio dhidi ya afya linalokuza siku hadi siku , na mimi na wenzangu wa Sekretarieti ya WHO tunafuatilia kwa umakini kabisa tishio hilo”.

Habari zilisema kuwa kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na WHO, katika wiki sita zilizopita, nchi na sehemu karibu 50 zisizokuwa na maambukizi ya virusi hivyo zimeripoti watu zaidi 3200 waliothibitishwa kuambukizwa virusi vya Monkeypox pamoja na mtu mmoja aliyekufa kutokana na virusi hivyo. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha