Utoaji wa simu zinazotumia teknolojia ya 5G wafikia milioni 17.74 nchini China Mwezi Mei

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 27, 2022

BEIJING - Takwimu kutoka Taasisi ya Teknolojia ya Upashanaji Habari na Mawasiliano ya Habari ya China (CAICT) zinaonyesha kuwa utoaji wa simu zinazotumia teknolojia ya 5G nchini China ulipanda kwa asilimia 6 kuliko wakati kama huo wa Mwaka jana hadi kufikia takriban simu milioni 17.74 Mwezi Mei mwaka huu.

Idadi hiyo ilichangia asilimia 85.3 ya utoaji wote wa simu za mkononi nchini China katika kipindi hicho, imesema CAICT, taasisi ya utafiti iliyo chini ya Wizara ya Viwanda na Teknolojia ya Habari ya China.

Katika miezi mitano ya kwanza ya mwaka huu, utoaji wa simu za mkononi nchini China ulipungua kwa asilimia 27.1 kuliko wakati huo wa Mwaka jana na kufikia simu milioni 108, ambapo kati ya hizo asilimia 79.7 zilikuwa simu zinazotumia teknolojia ya 5G.

China ilizalisha simu za kisasa milioni 106 katika kipindi cha Januari-Mei, ikiwa ni asilimia 98.2 ya jumla ya uzalishaji wake wa simu za mkononi katika miezi mitano ya kwanza.

Katika kipindi hicho, chapa za ndani pia zilichukua sehemu kubwa ya soko la simu za mkononi la China, ambalo lilichangia asilimia 83.8 ya jumla ya uzalishaji wa simu za mkononi nchini China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha