Sudan yazindua njia ya kwanza ya meli za baharini ya moja kwa moja kati yake na China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 28, 2022

Wasanii wa Sudan wakitumbuiza kwenye hafla ya uzinduzi wa njia ya meli za baharini huko Khartoum, Sudan, Juni 26, 2022. Sudan imefanya hafla ya uzinduzi wa njia ya kwanza ya meli za baharini ya moja kwa moja kati yake na China, katika Mji Mkuu Khartoum Jumapili jioni. (Picha na Mohamed Khidir/Xinhua)

KHARTOUM - Sudan imefanya hafla ya uzinduzi wa njia ya kwanza ya meli za baharini ya moja kwa moja kati yake na China, katika Mji Mkuu Khartoum Jumapili jioni.

Waziri wa Uchukuzi wa Sudan Hisham Ali Ahmed Abuzaid na Balozi wa China nchini Sudan Ma Xinmin ni miongoni mwa maafisa na wawakilishi wa wafanyabiashara wa nchi zote mbili waliohudhuria hafla hiyo.

Akibainisha kuwa Sudan iko Kaskazini-Mashariki mwa Afrika na kwenye pwani ya Magharibi ya Bahari ya Shamu, Ma amesema nchi hiyo inajivunia faida za kipekee za kijiografia na imekuwa njia kuu ya bidhaa za China kwenda Afrika tangu zamani.

Balozi huyo wa China ameongeza kuwa, Sudan na China zina uwezo mkubwa na matarajio mapana ya ushirikiano katika masuala ya usafirishaji wa majini.

“Meli ya mizigo yenye uwezo wa juu wa kubeba tani 32,000 ilianza safari yake ya kwanza kwenye njia mpya kutoka Bandari ya Sudan Juni 11, na inatarajiwa kufika katika kituo cha mwisho kwenye Bandari ya Qingdao, Mashariki mwa China, Julai 1,” amesema Xu Qun, Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kimataifa ya Uchukuzi ya Shanghai Greenroad, ambayo ni mwendeshaji wa meli hiyo.

Wawakilishi kutoka Sudan na China wakihudhuria hafla ya uzinduzi wa njia ya meli za baharini huko Khartoum, Sudan, Juni 26, 2022. (Picha na Mohamed Khidir/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha