Faida kwenye sekta ya viwanda ya China yaimarika kufuatia kurejea kwa shughuli za viwandani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 28, 2022

Mfanyakazi akifanya kazi kwenye karakana ya uzalishaji ya kiwanda cha kidijitali cha Xio Lift katika Wilaya ya Linping, Hangzhou, Mkoa wa Zhejiang nchini China Desemba 17, 2021. (Xinhua/Huang Zongzhi)

BEIJING – Takwimu rasmi kutoka Idara ya Taifa ya Takwimu ya China (NBS) zinaonesha kwamba faida ya makampuni makubwa ya viwanda nchini China ilipungua kidogo Mwezi Mei wakati viwanda katika nchi ya China ya pili kwa uchumi mkubwa duniani vikianza tena uzalishaji huku hisia za biashara zikiimarika.

Kwa mujibu wa takwimu hizo za NBS makampuni makubwa ya viwanda, kila moja ikiwa na mapato ya kibiashara ya angalau Yuan milioni 20 (kama dola za Kimarekani milioni 2.99), faida zao zilipungua kwa asilimia 6.5 Mwezi Mei kuliko mwaka jana wakati kama huo, ikipungua kutoka asilimia 8.5 ya Mwezi Aprili.

Takwimu hizo zinaonesha kuwa, mapato ya makampuni haya makubwa kwa mwezi uliopita wa Mei yalipanda kwa asilimia 6.8 kutoka mwaka mmoja uliopita, ikiwa ni kasi kubwa ya ukuaji ikilinganishwa na Aprili.

“Uchumi wa viwanda wa China unatengemaa na kuimarika” Xin Guobin, Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda na Teknolojia ya habari wa China amesema.

Akizungumzia takwimu hizo za Mwezi Mei, Mtakwimu Mkuu wa NBS Zhu Hong amehusisha upunguaji huo mdogo wa faida na udhibiti mzuri wa janga la Virusi vya Korona, kurejesha shughuli za biashara na maendeleo yaliyopatikana katika kuleta urahisi kwa shughuli za usafirishaji na uchukuzi.

Takwimu za NBS zinaonesha kuwa katika miezi mitano ya kwanza ya Mwaka huu, makampuni makubwa ya viwanda yalipata faida ya jumla ya takriban yuan trilioni 3.44, ikiongezeka kwa asilimia 1 kutoka mwaka mmoja uliopita.

Kati ya shughuli zote 41 za viwanda, 20 zilisajili ukuaji wa faida wa kila mwaka au kupunguza kwa kiasi kidogo faida ya Mwezi Mei kuliko mwaka jana wakatai kama huo, huku tano kati ya hizo zikifanikiwa kubadili mwelekeo wa kupungua kwa upanuzi wa baada ya kupata faida.

Ikichochewa na usaidizi wa kisera na bei ya juu kiasi, sekta ya nishati ilishuhudia faida ikiongezeka Mwezi Mei. Faida za viwanda vya unyonyaji wa makaa ya mawe, mafuta na gesi asilia iliongezeka zaidi ya maradufu, na hivyo kuchangia asilimia 9.5 ya ukuaji wa jumla wa faida ya viwanda mwezi uliopita.

Licha ya mabadiliko hayo mazuri, Zhu ametahadharisha kwamba kutokana na msingi dhaifu wa ufufukaji wa uchumi na mabadiliko ya mazingira ya kimataifa, bado kuna mambo mengi ya kutokuwa na uhakika kwa makampuni ya viwanda kupata faida.

Akizungumzia mwenendo huo wa sekta ya viwanda ya China, Zheng Houcheng, Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Usalama ya Yingda amesema, kwa kuzingatia kasi hiyo ya Mwezi Mei, kuna uwezekano mkubwa kwamba makampuni ya viwanda ya China yataripoti faida bora zaidi Mwezi Juni.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha