China yasema Marekani inapaswa kuwajibika kwa kutengeneza "mtego wa madeni"

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 28, 2022

BEIJING - Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Zhao Lijian jana Jumatatu alisema kuwa, kuita Mpango unaopendekezwa na China wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” ni mtego wa madeni ni hadithi ya uwongo, na ni Marekani ambayo inapaswa kuwajibishwa kwa kutengeneza "mtego wa madeni."

Zhao ameyasema hayo katika mkutano na waandishi wa habari wa kila siku alipokuwa akijibu shutuma za Marekani dhidi ya pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia moja”.

"Kuita pendekezo la 'Ukanda Mmoja, Njia moja' ni mtego wa madeni, hii ni hadithi ya uwongo," Zhao amesema.

Amesisitiza kuwa, kwa miaka tisa tangu kuanzishwa kwake, ujenzi wa “Ukanda Mmoja, Njia moja” umefuata kanuni ya mashauriano ya kina, mchango wa pamoja na manufaa ya pamoja na kufikisha manufaa yanayoonekana kwa nchi washirika wenzi na watu wake.

“Kwa mujibu wa makadirio ya Benki ya Dunia, ikiwa miradi yote ya miundombinu ya usafiri chini ya ujenzi wa “Ukanda Mmoja, Njia moja” itatekelezwa, ifikapo Mwaka 2030, ujenzi huo utazalisha mapato kwa Dunia yanayofikia dola za kimarekani trilioni 1.6, au asilimia 1.3 ya Pato la Dunia. Mapato yanayofikia hadi asilimia 90 yatakwenda kwa nchi washirika.” Zhao amesema.

Ameeleza kuwa ujenzi wa “Ukanda Mmoja, Njia moja” unaweza kuchangia katika kuwainua watu milioni 7.6 kutoka kwenye umaskini uliokithiri na milioni 32 kutoka kwenye umaskini wa wastani kutoka Mwaka 2015 hadi 2030.

"Kwa kweli, hakuna mshirika mwenzi wa ujenzi wa 'Ukanda Mmoja, Njia moja' aliyekubali tuhuma hiyo inayoitwa 'mtego wa madeni'. Badala yake, ni Marekani ambayo inapaswa kuwajibika kwa kutengeneza 'mtego wa madeni'," amesema msemaji huyo.

Zhao amesema kuwa sera panuzi za kifedha za Marekani, uvumbuzi wa kifedha wenye usimamizi uliolegea na uuzaji wa muda mfupi ulio na nia mbaya vinalemea nchi zinazoendelea na mzigo wa madeni na ndiyo sababu yenyewe inayozifanya baadhi ya nchi kuingia kwenye mtego wa madeni.

Kuhusiana na mpango mpya uliotolewa na G7, Zhao amesema China daima inakaribisha mipango inayohimiza miundombinu ya kimataifa. Mipango kama hii siyo lazima kushindana kila mmoja.

"Tunachopinga ni hatua za kuendeleza hesabu za siasa za kijiografia na kuipaka matope ujenzi wa “Ukanda Mmoja, Njia moja” kwa jina la kuhimiza maendeleo ya miundombinu," ameongeza.

"Pia niliona kwamba mwaka mmoja uliopita, ilikuwa pia katika Mkutano wa G7 ambapo Marekani iliweka mbele Pendekezo la B3W. Marekani ilijitolea wakati huo kuendeleza miundombinu ya kimataifa kwa njia iliyo tofauti na BRI. Iwe B3W au mipango mingine yoyote, Dunia inataka kuona uwekezaji wa kweli na miradi ambayo italeta manufaa kwa watu,” Zhao amesema.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha