Majaribio ya upandaji wa mbegu za China za mpunga unaoweza kuokoa maji na kustahimili ukame yapata mafanikio Botswana

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 29, 2022

Tarehe 27, shughuli ya “siku ya mavuno ya mpunga wa China” ilifanyika nchini Botswana ili kupongeza mafanikio ya upandaji wa mbegu za China za mpunga unaoweza kuokoa maji na kustahimili ukame nchini Botswana.

Juni 27, Kaimu Rais wa Botswana Tsochowane akivuna mpunga unaoweza kuokoa maji na kustahimili ukama uliotokana na mbegu za China huko Gaborone. (Xinhua)

Siku hiyo, balozi wa China nchini Botswana Wang Xuefeng na Kaimu Rais wa Botswana Tsochowane walifika kwenye mashamba ya majaribio ya upandaji wa mpunga, wakichukua mundu walivuna mpunga na kufurahia pamoja mavuno. Watu hao wawili pia walibadilishana mawazo kuhusu kuimarisha ushirikiano kati ya nchi zao mbili katika sekta ya kilimo.

Mpunga uliovunwa siku hiyo ulipandwa kwa majaribio chini ya ushirikiano kati ya Chuo Kikuu cha Kilimo na Maliasili cha Botswaa na Kampuni ya Kilimo cha Afrika ya Botswana, zikichagua mbegu za China za mpunga unaoweza kuokoa maji na kustahimili ukame, kuanza upandaji wa majaribio nchini Botswana ili kupata mpunga unaofaa kwa hali ya hewa ya Botswana na kuenea nchini kote.

Kaimu Rais wa Botswana Tsochowane alisema kuwa mafanikio hayo ya upandaji wa mbegu za mpunga za China yana umuhimu mkubwa kwa Botswana kuongeza uzalishaji wa nafaka, kupunguza utegemezi wa kuagiza nafaka kutoka nje, na kuhakikisha usalama wa chakula.

 Alisema, China ina teknolojia ya hali ya juu na uzoefu mkubwa katika uzalishaji wa kilimo na anatarajia nchi hizo mbili kuimarisha zaidi ushirikiano katika sekta ya kilimo.

Picha hii iliyopigwa Juni 27 ikionesha mashamba ya majaribio ya upandaji wa mbegu za China za mpunga unaoweza kuokoa maji na kustahimili ukame huko Gaborone, Botswana. (Xinhua)

Wang Xuefeng alisema kuwa upande wa China ungependa kujiunga pamoja na upande wa Botswana katika kuendeleza kwa kina ushirikiano kati ya nchi hizi mbili katika kilimo, kunufaika pamoja na uzoefu wa China katika kuhakikisha usalama wa chakula, kusaidia Botswana kufanya utafiti wa kina wa kisayansi kuhusu mazao ya nafaka ukiwemo mpunga unaostahimili ukame, ili kuisaidia Botswana katika kazi za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, kuboresha kiwango cha uzalishaji wa kilimo, kutimiza mapema kujitosheleza kwa chakula, na kufanya vitendo halisi kwa kuleta manufaa zaidi kwa wakulima wa Botswana.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha