Barabara Kuu iliyojengwa na China nchini Algeria yasifiwa kwa ubora wa hali ya juu na mchango wake

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 29, 2022

ALGIERS - Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Barabara Kuu nchini Algeria Mohamed Khaldi siku ya Jumanne wiki hii amesifu mradi wa barabara kuu uliojengwa na China kwa kuwa na ubora wa kiwango cha juu na mchango wake katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya nchi hiyo.

Khaldi amesema mradi huo wa barabara yenye urefu wa Kilomita 53 uliotekelezwa na Shirika la Uhandisi wa Ujenzi la China (CSCEC), umewezesha ipasavyo maendeleo ya kijamii na kiuchumi, kuokoa gharama za usafirishaji, na kuboresha urahisi wa usafiri kwa wenyeji.

Khaldi ameyasema hayo alipoungana na wajumbe wa Kamati ya Mawasiliano ya Barabara Kuu ya Trans-Sahara kutembelea sehemu ya kilomita 53 za barabara hiyo ya kuingilia Barabara ya Trans-Sahara, ambao ni mradi wa Bara la Afrika unaounganisha nchi sita za Afrika, ambazo ni Algeria, Chad. Mali, Niger, Nigeria, na Tunisia.

Ikiwa na urefu wa jumla ya zaidi ya Kilomita 9,000, njia hiyo ya barabara kuu ni sehemu ya Barabara ya kutoka Algiers hadi Lagos, Nigeria ambayo ina urefu wa Kilomita 4,500. Mradi huo kabambe unalenga kuzipa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara ufikiaji wa Bahari ya Mediterania. Pia unalenga kuongeza ushirikiano wa kiuchumi na mabadilishano ya kibiashara baina ya nchi za Afrika, pamoja na kuharakisha uunganishaji wa kikanda na kimataifa.

Kwa sababu ya maeneo yenye mwinuko na miradi ikijumuisha ujenzi wa handaki lenye urefu wa kilomita 9.6 na daraja lenye urefu wa kilomita 2.7, sehemu ya barabara kuu hiyo yenye urefu wa kilomita 53 inayounganisha miji ya Kaskazini mwa Algeria ya Chiffa na Berrouaghia inachukuliwa kuwa moja ya sehemu zenye changamoto na ngumu zaidi za barabara kuu nzima.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na kampuni hiyo ili kujenga sehemu hiyo, CSCEC imetengeneza zaidi ya ajira 10,000 nchini Algeria na kutoa mafunzo kwa zaidi ya wataalamu 2,000 katika sekta ya ujenzi.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha