China yaitaka G7 kusitisha mashambulizi yote na kashfa dhidi yake

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 30, 2022

BEIJING - China siku ya Jumatano ililitaka Kundi la nchi saba zenye maendeleo ya viwanda duniani (G7) kuacha kuishambulia na kuipaka matope, na kuacha aina zote za kuingilia mambo ya ndani ya China, kufuata taarifa iliyotolewa hivi karibuni kwenye mkutano wa kilele wa G7 ikitoa tuhuma za uzushi kuhusu masuala yanayohusiana na China.

Akibainisha kuwa tamko la G7 linavumisha hadithi ya "demokrasia dhidi ya udikteta" na kuzusha makabiliano, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Zhao Lijian amesema hii inathibitisha kikamilifu kwamba G7 haina nia ya kufanya mazungumzo na ushirikiano kwa misingi ya usawa na heshima, badala yake, inashikilia mawazo ya Vita Baridi na upendeleo wa kiitikadi, ikigeukia siasa za kambi kwa kuzingatia masilahi ya "vikundi vyao vidogo."

Kuhusu masuala ya Hong Kong, Zhao amesema kuwa, tangu Hong Kong irudi China, haki na uhuru wa kidemokrasia unaofurahiwa na wakazi wa Hong Kong kwa mujibu wa sheria vimehakikishwa kikamilifu. Serikali ya China imeiongoza Hong Kong kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Watu wa China na Sheria ya Msingi ya Hong Kong.

"Zikiwa zimechafuliwa kote, nchi hizi hazina nafasi ya kuwa 'mhadhiri' wa masuala ya haki za binadamu, na bado hazina haki ya kutumia haki za binadamu kama chombo cha kisiasa kuingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine," ameongeza.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari wa kila siku, Zhao amesema kuwa kuna China moja tu duniani na Taiwan ni sehemu isiyoweza kutengwa ya ardhi ya China. Shughuli za kuifanya "Taiwan ijitenge" na jaribio la nchi fulani "kuitumia Taiwan kuizuia China" ni tishio kubwa kwa amani na utulivu kwenye Mlango-Bahari wa Taiwan, amesema.

"China ina haki ya kuchukua hatua zote muhimu ili kulinda kwa uthabiti mamlaka ya nchi na usalama wa taifa," Zhao ameongeza.

Msemaji huyo amesema China siku zote imekuwa ikifuata kwa bidii malengo na kanuni za Katiba ya Umoja wa Mataifa, ikisimama kama mtetezi thabiti wa amani na maendeleo ya Dunia, pamoja na usalama na utulivu wa kikanda, kinyume kabisa na Marekani, ambayo imekuwa ikiendesha vita kote duniani na mara kwa mara ikiamua kuweka vikwazo vya upande mmoja.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha