Quan Hongchan na Bai Yuming watwaa medali ya dhahabu ya 100 ya Mashindano ya uogeleaji ya dunia kwa Timu ya China ya kupiga mbizi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 30, 2022

Katika fainali ya mchezo wa kupiga mbizi pamoja kwa mchezaji wa kike na mchezaji wa kiume katika Mashindano ya uogeleaji ya Dunia ya Mwaka 2022 yanayofanyika huko Budapest, mchezaji mdogo mwenye umri wa miaka ya 15 Quan Hongchan alishiriki pamoja na mwenzake Bai Yuming na walitwaa ubingwa kwa alama 391.40 ambayo wamepata medali ya dhahabu ya 100 kwenye Mashindano ya uogeleaji ya dunia kwa Timu ya China ya kupiga mbizi.

  

Juni 29, Quan Hongchan (kushoto) na Bai Yuming wakipiga picha pamoja baada ya hafla ya kutoa medali. (Picha na Xinhua)

“Ninafurahi sana kupata medali ya dhahabu, kwa sababu ni mara yangu ya kwanza kushiriki kwenye Mashindano ya Uogeleaji ya Dunia. Sijafanya vizuri sana katika mashindano hayo ya mchezo .” Bai Yuming alisema kwa unyenyekevu.

Quan Hongchan aliyeshiriki kwenye mashindano hayo badala ya mwenzake wakati wa mahitaji ya muda alisema baada ya mchezo kuwa "Nilishangaa na kufurahi sana wakati nilipoitwa kushiriki kwenye mchezo wa kupiga mbizi pamoja na mwenzangu wa kiume . Wakati wa kushiriki kwenye mashindano ya mchezo, sikufikiria sana alama ninayoweza kupata, lakini wakati wachezaji wengine walipopiga mbizi , nilitazama kwa makini, hasa mwenzangu Bai Yuming, nikitumai moyoni mwangu kwamba angeweza kucheza vizuri zaidi. Ninaona sisi sote tulicheza vizuri leo.”

Wachezaji wa Timu ya Ufaransa Gillet/Jeandal walishinda medali ya fedha kwa alama ya 358.50 na wachezaji wa Timu ya Uingereza Spendolini-Cirière/Hitley walichukua nafasi ya tatu kwa alama ya 357.60.

Juni 29, Quan Hongchan akicheza mchezo. (Picha na Xinhua)

Juni 29, Bai Yuming akicheza mchezo. (Picha na Xinhua)

Juni 29, Quan Hongchan (kushoto) na Bai Yuming wakipiga picha pamoja baada ya hafla ya kutoa medali. (Picha na Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha