China yafuta alama ya tahadhari kwenye alama ya usafiri wa mtu wakati wa kudhibiti maambukizi ya korona

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 30, 2022

Msafiri akionesha alama yake ya afya kabla ya kuingia kituo cha sabwe cha Beijing, Mei 17, 2022. (Picha/Xinhua)

China imetangaza kuwa kuanzia Jumatano wiki hii alama ya tahadhari imeondolewa kwenye alama ya kumbukumbu za usafiri wa mtu katika wakati wa kudhibiti maambukizi ya UVIKO-19.

Wizara ya Viwanda na Upashanaji Habari ilisema, hatua hiyo mpya inalenga kutekeleza sera ya kuzuia wagonjwa kutoingia China kutoka nje, kuzuia kuibuka tena kwa maambukizi nchini humu, na kutekeleza sera ya “maambukizi sifuri ya UVIKO”.

Wizara ya Afya ya China ilisema, hatua hiyo pia inalenga kuunga mkono uratibu wenye ufanisi kati ya udhibiti wa maambukizi na maendeleo ya jamii na uchumi, pamoja na kurahisisha usafiri wa watu.

Katika siku zilizopita, alama ya tahadhari iliweza kuonekana kwenye alama ya kumbukumbu za usafiri wa mtu, ili kuonesha usafiri wa mtu uliowahi kupita maeneo yenye hatari ya juu au ya kiwango cha kati ya maambukizi ya UVIKO-19.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha