Mashirika ya kimataifa yasema sekta ya mazao ya kilimo duniani itakabiliwa na changamoto za kimsingi katika miaka kumi ijayo

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 01, 2022

Shirika la Ushirikiano na Maendeleo ya Uchumi (OECD) na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) jana tarehe 29 yalitoa ripoti kwa pamoja kuhusu "Mtazamo wa Kilimo 2022-2031" na kudhihirisha kuwa sekta ya mazao ya kilimo kote duniani itakabiliwa na changamoto za kimsingi katika miaka kumi ijayo, ambapo itahitaji kuchukua hatua kwa njia endelevu kuwalisha watu ambao idadi yake inaongezeka siku hadi siku, na kukabiliana na changamoto za kukatika kwa usambazaji wa chakula kutokana na athari ya misukosuko ya hali ya hewa.

Hiki ni kibanda cha kuuza chakula huko Sana'a, Yemen, picha hii ilipigwa Juni 29. (Picha na Muhammad Mohamed/Xinhua)

Ripoti ilisema kuwa ufufukaji wa mahitaji baada ya maambukizi ya virusi vya korona, hali mbaya ya hewa katika nchi muhimu za utoaji wa mazao, na kupanda kwa gharama za uzalishaji na usafirishaji, sababu hizo zote zimeshapandisha bei za mazao ya kilimo, ambapo uuzaji usio na uhakika wa mazao ya kilimo kutoka Ukraine na Russia ambazo ni nchi muhimu zaidi za utoaji wa nafaka umeifanya hali ya hivi sasa izidi kuwa mbaya.

Mkurugenzi Mkuu wa FAO Qu Dongyu alisema kupandishwa kwa bei za chakula, mbolea na nishati, pamoja na hali ngumu ya mambo ya fedha, hayo yanawafanya watu wengi kukumbwa na taabu maishani. Kama hali ya usambazaji wa chakula kote duniani itazidi kuwa mbaya kutokana na kupungua kwa utoaji wa mazao wa nchi muhimu za uzalishaji wa mazao, idadi ya watu watakaokabiliwa na utapiamlo duniani kote inakadiriwa kuongezeka kwa zaidi ya milioni 19 ifikapo mwaka 2023.

Hizi ni nafaka zinazotazamiwa kuuzwa huko Sana'a, Yemen, picha hii ilipigwa Juni 29. (Picha na Muhammad Mohamed/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha