China yaitaka Marekani kuacha kukandamiza makampuni kutoka China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 01, 2022

BEIJING – Wizara ya Biashara ya China Alhamisi wiki hii imesema kwamba Marekani inapaswa kurekebisha mara moja makosa yake na kuacha kuwekea vikwazo na kukandamiza makampuni ya China.

Shu Jueting, Msemaji wa wizara hiyo ameyasema hayo kwenye mkutano na waandishi wa habari wakati akijibu hatua za hivi majuzi za Marekani za kuwekea vikwazo makampuni husika ya China kwa visingizio vinavyohusiana na uhusiano na Russia, Iran, na wa kijeshi.

Shu amesema, kwa kile kinachoitwa "kulinda utaratibu wa kimataifa," vitendo kama hivyo, kimsingi, ni vitendo vya upande mmoja, kujilinda kiuchumi, na ubabe, na kwa kawaida ni mabavu ya kiuchumi.

Vitendo hivyo vinaathiri vibaya utaratibu wa kimataifa wa kiuchumi na sheria za biashara na kutishia uthabiti wa minyororo ya kimataifa ya viwanda na ugavi. Pia vinaharibu masilahi muhimu ya makampuni duniani , yakiwemo makampuni ya China na Marekani, Shu amesema huku akiweka wazi kuwa China inapinga vikali.

Shu amesema China itachukua hatua zinazohitajika ili kulinda kwa uthabiti haki na maslahi halali ya makampuni ya kibiashara ya China na kulinda mamlaka ya nchi, usalama na maslahi ya maendeleo.

"Tunatumai kuwa Marekani inaweza kukutana na China katikati na kufanya mambo mengi zaidi kwa ajili ya uthabiti wa minyororo ya kimataifa ya viwanda na ugavi na ufufukaji wa uchumi," Shu amesema.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha