Hotuba ya Rais Xi Jinping yasifiwa kwa kutoa mwelekeo wa mustakabali mzuri wa Hong Kong

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 04, 2022

Picha iliyopigwa Juni 30, 2022 ikionyesha mapambo ya umbo la meli ya kuadhimisha miaka 25 tangu Hong Kong irudi China huko Hong Kong, China. (Xinhua/Li Genge)

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping siku ya Ijumaa ya wiki iliyopita alitoa hotuba kwenye mkutano wa kuadhimisha miaka 25 ya Hong Kong kurejea kwa China na hafla za kuapishwa kwa serikali ya awamu ya sita ya Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong.

Wataalam na wanataaluma wa nchi mbalimbali wamesema hotuba hiyo ya Xi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China, imefafanua umuhimu wa kufuata kanuni ya "nchi moja, mifumo miwili", na kutoa mwelekeo wa mustakabali mzuri wa Hong Kong.

Picha ya panoramiki iliyopigwa Septemba 12, 2020 kutoka angani ikionyesha Daraja la Hong Kong-Zhuhai-Macao, China. (Xinhua/Chen Yehua)

Nafasi bora katika maendeleo

"Tangu kurejea kwake kwa China, katika mchakato wa kufanya mageuzi na kufungua mlango nchini China, Hong Kong imekuwa ikijenga msingi mpya, ikifanya kazi kama daraja muhimu kati ya China Bara na Dunia nzima. Kutokana na hali hiyo, imetoa mchango usioweza kubadilishwa.” Xi alisema katika hotuba yake kwenye mkutano huo.

Stephen Perry, Mwenyekiti wa Klabu ya Vikundi 48 ya Uingereza, amesema "China pamoja na nchi za Asia, ina ukuaji bora zaidi, asilimia 30 ya ongezeko la uchumi wa Dunia inatoka China."

Kama sehemu ya China, Hong Kong ina jukumu muhimu sana, Perry amesema, akibainisha kuwa Eneo la Ghuba pana ya Guangdong-Hong Kong-Macao Greater "litakuwa eneo linaloongoza nchini China."

Rais wa China katika hotuba yake alisema kwamba "Iwe ni msukosuko wa mambo ya fedha duniani, janga la UVIKO-19, au machafuko ya kijamii, hakuna hata moja lililozuia Hong Kong kusonga mbele."

Bendera ya Taifa ya China na ile ya Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong (HKSAR) zikipepea kwenye Barabara ya Lee Tung huko Hong Kong, China, Juni 28, 2022. (Xinhua/Li Gang)

Ushikiliaji wa muda mrefu wa “nchi moja, mifumo miwili”

Akisisitiza kwamba "nchi moja, mifumo miwili" "hutumikia masilahi ya kimsingi siyo tu ya Hong Kong na Macao, bali pia nchi nzima na taifa," Xi alisema katika hotuba yake kwamba "Hakuna sababu ya sisi kubadili sera nzuri kama hiyo, na lazima tuifuate kwa muda mrefu."

Akirejelea maneno ya Xi, Masood Khalid, balozi wa zamani wa Pakistan nchini China, amesema mafanikio ya kiuchumi ya Hong Kong na ukweli kwamba inaunganishwa kikamilifu na China Bara na soko la kimataifa ni uthibitisho wa mafanikio ya utekelezaji wa kanuni ya "nchi moja, mifumo miwili."

Picha iliyopigwa Juni 25, 2022 ikionyesha hali ya taa za rangi zinazoangaza usiku huko Tsim Sha Tsui, Hong Kong, China. (Xinhua/Wang Shen)

Mustakabali mzuri wa baadaye

"Ninaweza kusema kwa ujasiri kwamba nimeshuhudia maendeleo ya sekta ya biashara ya Hong Kong," Dewan Saiful Alam Masud, Rais wa Shirikisho la Wafanyabiashara wa Bangladesh la Hong Kong, ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua.

Ameeleza kuwa, hotuba ya Rais Xi imetoa faraja na hakikisho kwa Hong Kong.

"Kwa uungaji mkono muhimu kutoka kwa serikali kuu, nina hakika kwamba fursa muhimu kwa watu wa Hong Kong na biashara zitaibuka, na hivyo kuruhusu Hong Kong kupiga hatua kubwa kuelekea kuibuka kama kituo cha biashara chenye nguvu zaidi na cha kuvutia zaidi," Masud amesema. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha