Ufunguzi wa Jumba la Makumbusho la Kasri ya Ufalme la Hong Kong wasifiwa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 04, 2022

Watalii wakiangalia vyombo vya kauri na hazina nyingine za taifa kwenye Jumba la Makumbusho la Kasri ya Ufalme la Hong Kong linalofunguliwa kwa umma Jumapili ya wiki iliyopita. (Picha/ChinaDaily)

Jumba la Makumbusho la Kasri ya Ufalme la Hong Kong lilifunguliwa kwa umma Jumapili ya wiki iliyopita, likichochea uchangamfu na fahari wa wakazi wa mji huo kwa utamaduni wa taifa na historia yake ya miaka 5000. Watalii wengi wamesema maonyesho hayo hayasahauliki na yanastahili kutembelewa tena.

Ili kuadhimisha miaka 25 ya kurudi China kwa Hong Kong, jumba hilo jipya la kitamaduni limeonesha sanaa 900 zenye thamani kubwa zilizoazimwa kutoka Jumba la Makumbusho la Kasri ya Ufalme la Beijing. Baadhi ya sanaa hizo hazijawahi kuoneshwa kwa umma.

Kutokana na hali joto ya hewa, ufunguzi wa jumba hilo umeahirishwa kutoka Jumamosi hadi Jumapili.

Baada ya kungoja kwa siku nzima, matarajio ya watalii yamefikia juu zaidi. Saa 2 asubuhi ya siku hiyo, yaani saa moja kabla ya ufunguzi, wakazi wa Hong Kong walikuwa wamekuwapo foleni kwa furaha mbele ya jumba hilo.

Mkazi wa Hong Kong mwenye umri wa miaka 29 Timothy Chan, ambaye anapenda kutembelea jumba la makumbusho alisema, kuwa ni jambo lisilosahaulika kwa kikundi cha kwanza cha watalii wanaotembelea jumba hilo. Alisema aliwahi kupanda ndege na kutembelea jumba la makumbusho la kasri ya ufalme la Beijing, lakini hivi sasa ni ngumu kwake kwenda Beijing tena kwa sababu ya maambukizi ya UVIKO-19. Ufunguzi wa Jumba la Makumbusho la Kasri ya Ufalme unatoa chaguzi jipya kwake.

Chan alisema, alama hiyo mpya ya utamaduni ya Hong Kong siyo tu imeleta uhondo wa utamaduni kwa watu wanaopenda majumba ya makumbusho kama yeye, bali pia itasaidia kuchochea matarajio ya wakazi ya kufahamu zaidi utamaduni wa China.

Jumba hilo la makumbusho lilisema, hadi jumamosi ya wiki iliyopita, tiketi 115,000 hivi zilikuwa zimenunuliwa, ambazo zimechukua asilimia 85 ya tiketi zote zilizonunuliwa Julai.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha