Rais Xi Jinping atoa wito wa kuweka maendeleo mbele na msingi katika ajenda za kimataifa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 05, 2022

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping Jumatatu wiki hii amesema kuwa China iko tayari kushirikiana na nchi duniani kote kuweka maendeleo mbele na msingi katika ajenda za kimataifa.

Rais Xi ameyasema hayo katika barua ya pongezi kwa kongamano la maendeleo ya kimataifa lililohudhuriwa na wajumbe wa jumuiya ya washauri mabingwa na wa vyombo vya habari mjini Beijing, China.

Xi amesema, hivi sasa, Dunia inakabiliwa na athari mbili za mabadiliko makubwa na janga hatari la UVIKO-19, ufufukaji wa uchumi wa Dunia ni dhaifu, na kuna pengo linaloongezeka kati ya nchi za Kaskazini na Kusini.

"Wakati Dunia inaingia katika kipindi kipya cha misukosuko na mabadiliko, kuhimiza maendeleo imekuwa mada kuu inayowakabili binadamu," Xi amesema. "Kwa hiyo, China imetoa Pendekezo la Maendeleo ya Dunia."

China iko tayari kushirikiana na nchi mbalimbali duniani katika kufuata wazo la kutafuta maendeleo kwa ajili ya umma, na kushikilia kufanya ushirikiano wa pande nyingi na kuleta manufaa kwa wote, kutafuta maendeleo yanayotokana na uvumbuzi, na kutafuta maendeleo katika hali ya kupatana kati ya binadamu na mazingira ya asili.

Amesema, China pia iko tayari kusukuma kuweka maendeleo mbele na kuwa msingi katika ajenda za kimataifa, kuharakisha utekelezaji wa Ajenda ya Umoja wa Mataifa ya Mwaka 2030 ya Maendeleo Endelevu, na kuhimiza maendeleo ya dunia nzima yawe na nguvu na kijani zaidi, na mazuri zaidi.

Barua ya Xi ilisomwa kwenye kongamano hilo na Huang Kunming, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mkuu wa Idara ya Uenezi ya Kamati Kuu ya CPC, ambaye pia alitoa hotuba kwenye hafla hiyo.

Kongamano la "Maendeleo ya Dunia: Jukumu la Pamoja na Thamani ya Vitendo" kwa ajili ya jumuiya ya washauri mabingwa na vyombo vya habari liliandaliwa na Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China.

Huang Kunming, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mkuu wa Idara ya Uenezi ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, akisoma barua ya pongezi ya Rais Xi Jinping wa China kwa Kongamano la "Maendeleo ya Dunia: Jukumu la Pamoja na Thamani ya Vitendo. " lililohudhuriwa na wajumbe wa jumuiya ya washauri mabingwa na vyombo vya habari na pia alitoa hotuba kwenye kongamano hilo lililofanyika Beijing, China, Julai 4, 2022. (Xinhua/Zhai Jianlan)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha