Kurejea tena kwa utalii kwaonesha Xinjiang ilivyostawi, imara na yenye maisha ya wazi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 06, 2022

URUMQI - Kwenye Barabara Kuu ya Duku iliyoko Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uygur, Kaskazini Magharibi mwa China, msururu mrefu wa magari, SUV na RV ndogo unaweza kuonekana ukipita maeneo mengi yenye mandhari ya kuvutia.

Barabara hiyo kuu yenye urefu wa kilomita 561 inayopitia Milima ya kuvutia ya Tianshan hufunguliwa tu kuanzia Juni hadi Oktoba kila mwaka na inaaminika kuwa ni njia nzuri zaidi nchini China.

Katika wiki za hivi majuzi barabara kuu hiyo imekabiliwa na hali ya kuongezeka kwa watalii wengi, huku magari yakimiminika kutoka kote mkoani humo.

Watalii wakitembelea shamba la lavenda lililoko eneo la Huocheng la Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uygur, Kaskazini-Magharibi mwa China, Juni 19, 2022. (Xinhua/Zhao Ge)

Utalii rahisi

Xinjiang inajumuisha ukubwa wa kilomita za mraba milioni 1.66 au takriban moja ya sita ya eneo lote la ardhi la China. Kusafiri hadi Xinjiang na kutembelea sehemu zake mbalimbali zenye vivutio ilikuwa kazi ngumu.

Hiyo, lakini, ni jambo la zamani. Leo, Xinjiang ina viwanja 24 vya ndege za abiria , huku kiwanja cha 24 kikifunguliwa mwezi uliopita, na vingine vipya vikiendelea kujengwa.

Kuna machaguo mengine ya usafiri yanayopatikana kwa wale wanaopenda kuchukua safari za barabarani, ili waweze kufurahia mandhari ya kuvutia njiani. Mwezi uliopita, Reli ya kati ya miji ya Hotan na Ruoqiang ilianza kutumika rasmi, ikiwa ni mwanzo wa uzinduzi wa njia ya kwanza ya reli ya jangwa duniani. Barabara kuu ya tatu inayopita Jangwa la Taklimakan nayo ilifunguliwa wiki iliyopita.

Mkoa huo pia umeboresha huduma ya malazi kwa watalii na miundombinu mbalimbali ya utalii.

Picha iliyopigwa kutoka angani ikionyesha barabara kuu mpya inayopita kwenye Jangwa la Taklimakan la Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uygur nchini China, Juni 23, 2022. (Xinhua/Gu Yu)

Uzoefu wa kutosha

Wu Beilei, mwongoza watalii mwenye uzoefu wa miaka 14, anasema amekuwa akitumia fikra zake nyingi kuleta mambo mapya mazuri anayoweza kuwapa wateja wake, mbali na kutembelea maeneo ya kitamaduni, kuendesha gari, kupanda milima na kupiga kambi.

"Miaka kumi iliyopita, watalii walikuja Xinjiang kupiga picha nzuri tu na kuziweka kwenye albamu. Sasa mahitaji yao yamebadilika kwa kiasi kikubwa," Wu amesema.

Hili limeibua uvumbuzi katika sekta ya utalii huko Xinjiang na kuchangia kuibuka na kukua kwa utalii wa maeneo, mandhari na utamaduni.

Watalii wakicheza kwenye vifaa vya kuteleza kwenye theluji katika eneo la mapumziko la Oynak, lililoko Moyu, Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang, Januari 9, 2022. (Xinhua/Ding Lei)

Nyuso za furaha

Dilnur Ablimit ni mmoja wa wamiliki wa biashara ndogo ndogo katika mji wa asili yake wa Kashgar ambaye anajipatia riziki kutokana na utalii. Anaendesha studio ya kupiga picha na hukodisha mavazi ya kitamaduni ya kabila la Wauygur kwa watalii kupigia picha, huku pia akiwasaidia kujipodoa.

"Nataka wateja wangu waone jinsi utamaduni wa Wauygur unavyovutia na kupata marafiki kupitia uzoefu huu wa kitamaduni," anasema mjasiriamali huyo mwenye umri wa miaka 24.

Takwimu rasmi zinaonyesha kuwa zaidi ya ajira mpya 54,000 zinazohusiana na utalii zimetolewa tangu Mwaka 2018, na watu milioni 1.5 wanafanya kazi katika tasnia za huduma husika. 

Watalii wakipiga picha kwenye hoteli zilizoko mji wa kale wa Kashgar, Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang nchini China, Tarehe 12 Juni 2022. (Xinhua/Ding Lei)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha