

Lugha Nyingine
China yafanya hafla ya kumbukumbu za miaka 85 ya vita vya nchi nzima vya kupambana na uvamizi wa Japan
Shughuli za Kitaifa za kumbukumbu za Wahanga wa Mauaji ya Nanjing zilifanyika Nanjing Desemba 14, Mwaka 2021.
BEIJING - China Alhamisi wiki hii imefanya hafla ya kumbukumbu za miaka 85 tangu kuanza kwa vita vya nchi nzima vya kupambana na uvamizi wa Japan.
Mnamo Julai 7, 1937, wanajeshi wa Japan walipiga mizinga dhidi ya mji wa Wanping na kuzusha tukio la Daraja la Lugou lililoshtusha dunia, kuashiria mwanzo wa uvamizi kamili wa Japani dhidi ya China, ambapo watu wa nchi nzima ya China walianza kupambana na uvamizi wa Japani.
Maonyesho maalum kuhusu vita hivyo vya upinzani yalifanyika Alhamisi mjini Beijing kwenye Jumba la Makumbusho ya Vita vya Upinzani dhidi ya Uvamizi wa Japan la Watu wa China.
Hafla imefanyika katika jumba hilo la makumbusho na watu wapatao 300 walishiriki kwenye hafla hiyo, wakiwemo wajumbe wa mashujaa na wanafamilia wa viongozi wa kijeshi na waliojitoa mhanga kwenye vita. Washiriki hao waliweka maua mbele ya picha za mashujaa na kutoa heshima zao kwa mashujaa hao waliofariki wakati wakipigana na uchokozi wa Japan.
"Ili kulinda taifa letu , watu wengi walimwaga damu na kupoteza maisha. Tunapaswa kuthamini ushindi mgumu uliopatikana, kusoma kwa bidii na kutoa mchango kwa nchi yetu," amesema Yang Yifan, mwanafunzi mwenye umri wa miaka 15 kutoka Mkoa wa Shanxi, baada ya kutazama maonyesho hayo.
Shughuli za kumbukumbu za tukio hilo pia zilifanyika katika sehemu nyingine za China.
Siku ya Alhamisi asubuhi, zaidi ya watu 100 walishiriki kwenye shughuli hizo mbele ya jumba la kumbukumbu kwenye eneo linalojiendesha la Zhijiang Dong, Mkoa wa Hunan katikati mwa China. Walitoa heshima ya kuwa kimya kwa muda kwa ajili ya mashujaa waliojitoa mhanga na wenzao waliokufa katika vita.
Kitabu kuhusu Eneo la Usalama la Nanjing kilichapishwa Alhamisi. Mwaka 1937, raia wa Ujerumani John Rabe na wageni kadhaa walifanya juhudi za kutenga sehemu moja kuwa eneo la usalama la kimataifa katika mji huo bila kujali hatari kwa maisha yao wenyewe, ambapo waliokoa zaidi ya Wachina 200,000 wakati wa uvamizi wa Japan.
Zhang Lianhong, mkurugenzi wa kituo cha masomo kuhusu mauaji ya kimbari ya Nanjing katika Chuo Kikuu cha Nanjing Normal, amesema, "Kupitia utafiti wa Ukanda wa Usalama wa Nanjing, hatupaswi tu kuthamini roho ya kibinadamu, lakini pia kufichua zaidi ukatili wa uvamizi wa wanajeshi wa Japan, kukanusha kwa ushahidi wa kutosha kauli za kipuuzi zilizotolewa na nguvu za mrengo wa kulia za Japan, kuzuia ufufuo wa kijeshi wa Japani, na kulinda amani ya kudumu ya Dunia."
Wang Fei, mpiganaji mkongwe wa vita vya kupinga uvamizi wa Japani mwenye umri a miaka 95 alimesema, "China imesimama na kuwa na mafanikio leo. Kizazi cha vijana kinapaswa kusoma na kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya ustawishaji wa taifa."
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma