

Lugha Nyingine
Ubalozi wa Tanzania nchini China wafanya shughuli ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Lugha ya Kiswahili kwenye mtandao wa intenati
Balozi wa Tanzania nchini China Bw.Mbelwa Kairuki akitoa hotuba kwenye shughuli ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Lugha ya Kiswahili kwenye mtandao wa intenati.
Juni 7, Ubalozi wa Tanzania nchini China ulifanya shughuli ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Lugha ya Kiswahili kwenye mtandao wa intaneti, Balozi wa Tanzania nchini China Bw.Mbelwa Kairuki, Balozi wa Oman nchini China Bw.Nasser Al Busaid, Kaimu Balozi wa Kenya nchini China Bw.Wameru Kimani walishiriki kwenye shughuli hiyo na kutoa hotuba.
Katika hotuba yake, Balozi Kairuki alisema kuwa Lugha ya Kiswahili ni lugha ramsi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Bunge la Pan Afrika , na pia ni moja ya lugha za Afrika zinazotumiwa na watu wengi zaidi duniani. Anafurahi sana kuona Kiswahili kinatumika nchini China kutoka Afrika na kufanya kazi muhimu katika sekta ya uchumi, biashara, elimu na utalii kati ya China na Afrika. Hadi sasa, vyuo vikuu sita vya China vimefungua kozi ya Lugha ya Kiswahili, na vyombo vya habari ikiwemo Tovuti ya Gazeti la Umma vinatoa habari kwa Kiswahili. Anaamini kuwa ushirikiano kati ya China na Afrika utaendelezwa kwa kina kwa kutegemea Lugha ya Kiswahili, na anatumai shughuli hiyo itakuwa fursa ya kuhimiza maendeleo ya lugha ya Kiswahili nchini China.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO), Bibi Azoulay, alitoa pongezi zake kwa kupitia video. Balozi Mdogo wa Tanzania mjini Guangzhou, vyombo vya habari na wajumbe wa walimu na wanafunzi kutoka vyuo vikuu pia walishiriki kwenye shughuli hiyo.
Novemba 23, 2021, Mkutano wa 44 wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa lilitangaza Tarehe 7 Julai ya kila mwaka kuwa Siku ya Kimataifa ya Lugha ya Kiswahili.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma