

Lugha Nyingine
China yashuhudia kuongezeka kwa uwekezaji wa miundombinu ya uhifadhi wa maji katika nusu ya kwanza ya mwaka
![]() |
Picha iliyopigwa kutoka angani Tarehe 11 Machi 2022 ikionyesha mradi wa kuhifadhi maji wa Dateng Gorge huko Guiping, Mkoa unaojiendesha wa kabila la wazhuang wa Guangxi, Kusini mwa China. (Xinhua/Cao Yiming) |
BEIJING - China imeshuhudia kuongezeka kwa uwekezaji wa miundombinu ya uhifadhi wa maji katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, huku nchi hiyo yenye uchumi wa pili kwa ukubwa duniani ikiongeza juhudi za kuimarisha ukuaji wa uchumi wake.
Kwa mujibu wa Wizara ya Rasilimali za Maji ya China, kuanzia Januari hadi Juni, uwekezaji kwenye miradi ya uhifadhi wa maji nchini China ulifikia yuan bilioni 444.9 (kama dola za Kimarekani bilioni 66.29), ikiwa ni ongezeko la yuan bilioni 165.9, au karibu asilimia 60, zaidi ya Mwaka 2021.
Nchi hiyo ilianzisha miradi mipya 14,000 ya kuhifadhi maji katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, ikijumuisha miradi 750, kila moja ikiwa na uwekezaji wa zaidi ya yuan milioni 100.
Mkutano wa mwezi Juni uliofanyika kwa pamoja kati ya Benki ya Umma ya China na Wizara ya Rasilimali za Maji ulisema miradi ya uhifadhi wa maji inaweza kusaidia kuvuta uwekezaji mkubwa na kuongeza nafasi kubwa za ajira katika muda mfupi. Inaweza pia kulinda usalama wa chakula, kuwezesha maendeleo ya kijani, na kupunguza majanga ya asili kwa muda mrefu.
China inatarajiwa kukamilisha uwekezaji wenye thamani ya zaidi ya yuan bilioni 800 katika ujenzi wa hifadhi za maji kwa Mwaka 2022.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma