

Lugha Nyingine
Wazee wa kikabila wa Marekani wakumbuka machungu waliyoyapata wakati wakisoma shule za bweni
Picha iliyopigwa Mei 17, 2022 ikionyesha maonyesho katika Jumba la Makumbusho ya Taifa la Wamarekani wa asili Waindian huko Washington D.C., Marekani. (Xinhua/Liu Jie)
NEW YORK, - Shirika la Habari la Associated Press (AP) limeripoti kuwa, wazee wa jamii zenye asili ya Marekani waliowahi kuwa wanafunzi katika shule za bweni za Wamarekani asilia zinazoungwa mkono na serikali wametoa ushahidi kuhusu magumu waliyovumilia, ikiwa ni pamoja na kupigwa, kuchapwa viboko, kushambuliwa kingono, kukatwa nywele kwa kulazimishwa na kupewa majina ya utani yenye maumivu.
"Walitoka katika majimbo tofauti na makabila tofauti, lakini walishiriki uzoefu wa kawaida wa kusoma katika shule ambazo ziliundwa kuwaondolea watu wa asili utambulisho wao wa kitamaduni," inasema ripoti hiyo ya wiki iliyopita.
"Sera za Serikali Kuu ya Marekani kuhusu shule za bweni kwa wanafunzi wenye asilia ya Marekani zimegusa kila mtu wa kiasili ninayemjua," amesema Waziri wa Mambo ya Ndani wa Marekani Deb Haaland, ambaye yeye mwenyewe pia ni wa Jamii ya Laguna Pueblo kutoka New Mexico na waziri wa kwanza wa baraza la mawaziri kutoka makabila yenye asili ya Marekani katika historia ya nchi hiyo.
"Mababu zangu walistahimili maovu ya sera za kubadilishwa asili za shule za bweni za Wamarekani asilia zilizotekelezwa na wizara ile ile ninayoongoza sasa. Hii ni mara ya kwanza katika historia kwa waziri wa baraza la mawaziri kuja mezani na akiwa na historia hii yenye machungu," amesema kwenye tukio la kutoa ushahidi.
Shirika la Haaland hivi karibuni lilitoa ripoti ambayo ilibainisha zaidi ya shule 400, ambazo zilitaka kuwabadilisha na kuwaingiza watoto wa asili ya Marekani kwenye jamii za wazungu katika kipindi kilichoanzia mwishoni mwa Karne ya 18 hadi mwishoni mwa miaka ya 1960.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma