

Lugha Nyingine
Mwanamichezo mlemavu wa Tanzania aapa kufanya vizuri zaidi kwenye mashindano ya michezo ya kimataifa
Yohana Assa Mwila, mwanamichezo mlemavu wa kunyanyua uzito akifanya maandalizi kwa Michezo ya Jumuiya ya Madola ya Birmingham 2022 huko Dar es Salaam, Tanzania, Juni 18, Mwaka 2022. (Picha na Herman Emmanuel/Xinhua)
Yohana Assa Mwila mwenye umri wa miaka 38 ni mwanamichezo mlemavu wa kunyanyua uzito ambaye alipoteza mguu wake wa kulia mwaka 1988 kwa kuumwa na nyoka mwenye sumu kali, na atawakilisha Tanzania kushiriki kwenye Michezo ya Jumuiya ya Madola ya Birmingham 2022 nchini Uingereza ambayo itafanyika kuanzia Julai 28 hadi Agosti 8.
Mwila alisema,mguu wake wa kulia ulikatwa baada ya kuumwa na nyoka mwenye sumu kali.
Aliongeza kuwa kukatwa mguu huo haukuwa mwisho wa maisha yake ambapo Mwezi Machi, 2019 aliamua kufanya mazoezi ya kunyanyua uzito kufuatia ushauri wa kocha wake, Nemes Albert Chiwalala mwenye umri wa miaka 55.
Mwila, mfanyabiashara wa viatu vilivyotumiwa katika soko la Kariakoo, alisema anafanya mazoezi mara nne kwa wiki na kila mazoezi huchukua saa mbili katika Kituo cha Michezo cha Ada Estates kilichopo Dar es Salaam, mji mkuu wa kibiashara wa Tanzania.
Zaidi ya hayo, Mwila alishukuru sana ubalozi wa China kwa msaada wake wa hivi karibuni wa kutoa kompyuta na laptop kwa Kamati ya Olimpiki ya Walemavu ya Tanzania, akisema msaada huo umekuja wakati unaofaa.
“Kompyuta na laptop zitatusaidia kupata mtandao wa intaneti na kufanya mawasiliano na idara nyingine za michezo duniani. Hapo zamani, tulikuwa tunasubiri bosi atumie laptop yake binafsi kupata mtandao wa intaneti. Lakini sasa hali imekuwa tofauti. Nashukru ubalozi wa China nchini Tanzania kwa mchango huo.”Mwila alisema.
Kocha wa Mwila, Bw. Chiwalala alisema alianza kutoa mafunzo ya mazoezi ya kunyanyua uzito kwa walemavu mwaka 2000, na kuongeza kuwa wanamichezo wawili walemavu aliowafundisha walipata nafasi na kushiriki kwenye Michezo ya Jumuiya ya Madola ya mwaka 2002 huko Manchester, Uingereza.
“Nina matumaini kuwa Mwila atapata mafanikio makubwa katika Michezo ya Jumuiya ya Madola ijayo," alisema Chiwalala.
Yohana Assa Mwila, mwanamichezo mlemavu wa kunyanyua uzito akifanya maandalizi kwa Michezo ya Jumuiya ya Madola ya Birmingham 2022 huko Dar es Salaam, Tanzania, Juni 18, Mwaka 2022. (Picha na Herman Emmanuel/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma