Zaidi ya watu 1,000 wafariki kutokana na joto kali nchini Hispania

(CRI Online) Julai 22, 2022

Wizara ya Afya ya Hispania imesema, watu 1,047 wamefariki kutokana na joto kali mwaka huu, ambapo nyuzijoto ilifikia 40 katika sehemu nyingi za nchi hiyo katika siku 10 zilizopita.

Joto kali limewaathiri zaidi wazee, ambapo watu 672 waliofariki ni wazee wenye umri wa zaidi ya miaka 85, huku watu 241 wakiwa na umri wa kati ya miaka 75 na 85, na wengine 88 waliofariki wakiwa na umri wa kati ya miaka 65 na 74.

Msemaji wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini Hispania Bea Hevella amesema, idadi ya vifo ni kubwa kwa watu wenye magonjwa ya mfumo wa moyo na wa kupumua.

Joto kali nchini Hispania lilianza Juni 11 mwaka huu na kudumu kwa wiki moja.

 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha