Maelezo ya Katuni: Siasa za mabavu za Marekani zakiuka haki za binadamu za wakimbizi na wahamiaji duniani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 22, 2022

(Katuni na Ma Hongliang)

Marekani inajidai kuwa ni “kinara wa demokrasia” na inapenda kujifanya “mwalimu” wa kuingilia kati mambo ya ndani ya nchi nyingine. Vitendo vyake vimechocheza mawimbi kadhaa ya wakimbizi na kusababisha maafa makubwa ya kibinadamu.

Marekani ni chanzo cha suala la wahamiaji na wakimbizi. Katika miaka isiyofikia 250 iliyopita tangu Marekani ilipoanzishwa, ni chini ya miaka 20 iliyopita tu ndiyo haikufanya operesheni za kijeshi nje ya nchi, na imeeneza vita dunia nzima. Takwimu kutoka mradi wa “gharama za vita” wa Taasisi ya Waston ya Chuo Kikuu cha Brown cha Marekani zinaonesha kuwa, baada ya tukio la “911”, “vita dhidi ya ugaidi” vilivyoanzishwa na Marekani vimesababisha watu milioni 38 hivi kukimbia maskani yao.

Marekani ni mkiukaji mkubwa wa haki za binadamu za wakimbizi. Ubaguzi wa rangi wa kimfumo wa Marekani umejikita kwenye jamii. Tangu maambukizi ya virusi vya korona yalipolipuka, wahamiaji na makundi ya watu wachache wamekumbwa na ubaguzi na uhalifu kutokana na chuki. Ukuta uliojengwa kwenye mpaka wa Marekani na Mexico, kuwafukuza wahamiaji kwa mabavu, na kuwaweka kizuizini wahamiaji na wakimbizi ndani ya vituo vyenye mazingira magumu kwa muda mrefu, na kutekeleza kwa nguvu sera ya "kutenganisha wazazi wahamiaji na watoto wao...... Uhalifu wa kukiuka haki za binadamu za wahamiaji na wakimbizi nchini Marekani hauhesabiki.

Marekani imeanzisha vita nyingi kwa kisingizo cha “demokrasia”, kwa hivyo nchi hiyo si “mwalimu” wala “jaji”. Inapokabiliwa na lawama kali kutoka kwa wahamiaji na wakimbizi wa nchi mbalimbali duniani, Marekani inatakiwa kukumbuka kuwa italaumiwa tu na historia. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha