

Lugha Nyingine
Rais wa Tanzania na Rais wa Kenya washiriki kwenye hafla ya uzinduzi wa Barabara ya Arusha
Julai 22, 2022, Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (tano wa kulia) na Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Muigai Kenyatta (tano wa kushoto) walishiriki kwenye hafla ya uzinduzi wa Barabara ya Arusha ambayo ni sehemu moja ya Barabara ya Kikanda ya Arusha-Holili/Taveta-Voi iliyofanyika Mjini Arusha. Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ilitoa taarifa ikisema kuwa Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Muigai Kenyatta walizindua rasmi Barabara ya Arusha yenye urefu wa kilomita 42.4. Barabara hiyo ni sehemu moja ya barabara ya Arusha-Holili/Taveta-Voi inayounganisha kaskazini mwa Tanzania na mji wa bandari wa Mombasa,Kenya. Ni kipindi cha kwanza cha mradi ambao ulijengwa kwa ajili ya kupunguza msongamano wa magari mjini Arusha, ambayo ni makao makuu ya EAC, na mji wa Moshi nchini Tanzania, pamoja na kukuza biashara ya ndani ya kanda hiyo. (Ofisi ya Rais wa Tanzania/kutolewa na Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma