

Lugha Nyingine
Watanzania watakiwa kuwaenzi mashujaa waliopigania uhuru ambao wameiaga Dunia
DAR ES SALAAM - Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan Jumatatu wiki hii amewataka wananchi wenzake kuendelea kuwakumbuka na kuwaenzi mashujaa waliopigania uhuru wa nchi hiyo ambao wamefariki Dunia.
“Uzalendo wao umetufanya tuwe hivi tulivyo leo,” amesema Rais Samia ambaye pia ni amiri jeshi mkuu wa majeshi ya Tanzania kwenye hotuba yake ya kuadhimisha Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa wa Tanzania kwa Mwaka 2022 mjini Dodoma, Mji Mkuu wa Tanzania.
“Ili kuwaenzi mashujaa waliofariki Dunia, Watanzania lazima waendelee kuimarisha amani, upendo, utulivu na mshikamano,” amesema Samia.
Kwenye maadhimisho hayo, Rais Samia alimuagiza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Mamlaka ya Mkoa wa Dodoma kutafuta ardhi kwenye mji mkuu huo kwa ajili ya ujenzi wa mnara wa kuwaenzi mashujaa walioaga Dunia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma