Xi Jinping atuma barua ya pongezi kwa Mkutano wa Pili wa Baraza la Amani na Usalama la China na Afrika

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 26, 2022

Tarehe 25, Julai, rais Xi Jinping wa China alituma barua ya pongezi kwa Mkutano wa pili wa Baraza la Amani na Usalama la China na Afrika.

Xi alisisitiza kuwa, China na Afrika ni marafiki wakubwa, wenzi wema na ndugu wanaosaidiana kwenye dhiki. Hivi sasa, mabadiliko makubwa yanatokea kwa kasi katika dunia, ambayo hayajatokea hapo katika karne iliyopita, ambapo maambukizi ya virusi vya korona bado yanaeneza, na changamoto za usalama za aina mbalimbali zinatokea moja baada ya nyingine, jamii za binadamu zinakabiliwa na changamoto ambazo hazijatokea hapo kabla. Kutimiza amani ya kudumu na usalama wa kote duniani ni matarajio ya pamoja ya watu wa China na Afrika. Siku zote China inaendeleza uhusiano kati yake na Afrika kwa kushikilia mtazamo sahihi kuhusu haki na faida na kufuata dhana ya udhati na uwazi. Ingependa kushirikiana na marafiki wa Afrika katika kushikilia mawazo kuhusu usalama wa pamoja, wa jumla, wa ushirikiano na wa endelevu, kulinda mfumo wa kimataifa ambao kiini chake ni Umoja wa Mataifa, kulinda usawa na haki ya kimataifa, kuhimiza utekelezaji wa pendekezo la usalama wa dunia, na kujenga jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja katika zama mpya.

Mkutano wa pili wa Baraza la Amani na Usalama la China na Afrika ulifanyika siku hiyo kwa njia ya video, ukiwa na kaulimbiu ya “Kuimarisha mshikamano na ushirikiano, na kutimiza usalama wa pamoja”, mkutano huo ambao uliandaliwa na Wizara ya Ulinzi ya China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha