

Lugha Nyingine
Watu wanaofanya kazi nje wakwepa joto kwenye mabasi yenye viyoyozi
Wafanyakazi wanaofanya kazi nje wakiondoka mabasi baada ya mapumziko huko Yichang, Mkoa wa Hubei wa Katikati mwa China Julai 16, 2022. (Picha/Xinhua)
Baada ya kufanya kazi nje yenye joto kali wakati wa asubuhi, adhuhuri mfanyakazi wa ujenzi wa mji Bw. Cai Kaijun alipanda basi lenye kiyoyozi bure linalosimama karibu na sehemu yake ya kufanya kazi ili kupumzika.
Katika wakati wa Mwezi wa Julai, joto kali limeathiri sehemu mbalimbali nchini China, ukiwemo mji wa Yichang, Mkoa wa Hubei wa Katikati mwa China, na limeleta changamoto kwa wafanyakazi wanaofanya kazi nje ya nyumba. Ili kuwawezesha kukwepa joto kali, Kampuni ya mabasi ya Yichang ilianzisha shughuli za hisani kuanzia Julai 8. Inaweka mabasi 9 katika sehemu 8 za mji huo kutoka saa sita hadi saa tisa mchana, ili kuwawezesha wafanyakazi hao wapumzike na kukwepa joto kali kwenye mabasi.
“Kwa sababu ya hali ya joto kali, hakuna abiria wengi wa mabasi adhuhuri. Kwa hivyo tunapanga mabasi ya ziada kwenye sehemu 8 karibu na mahali pa ujenzi wa mjini, ili wafanyakazi waweze kupumzika,” alisema Wang Jie, naibu meneja mkuu wa kampuni ya mabasi ya Yichang.
Mabasi hayo yanatoa mahitaji ya kawaida yakiwemo maji ya kunywa na dawa za kujikinga na hali joto. Madirishi ya mabasi yanafunikwa kwa mapazia ambayo yanalinda faragha za wafanyakazi. Licha ya hayo, mabasi mengi yanatumia nishati ya umeme, kwa hivyo hayapigi kelele na yanatoa mazingira kimya kwa mapumziko.
“Kila siku ninapumzika kwenye basi. Kwa kutegemea viyoyozi, ninajisia vizuri baada ya mapumziko,” alisema Cai.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma