Rais Xi Jinping wa China asisitiza juhudi zinazoendelea kufikia malengo ya karne ya PLA

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 29, 2022

Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) akitembelea maonesho ya mafanikio yaliyopatikana katika kuimarisha ulinzi wa nchi na majeshi katika zama mpya kwenye Jumba la Makumbusho ya Kijeshi la Mapinduzi ya Umma ya China, hapa Beijing, Mji Mkuu wa China, Julai 27, 2022. (Xinhua/Li Gang)

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amesisitiza juhudi za kuendelea kwa bidii ili kufikia malengo yaliyowekwa kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA).

Xi, aliyasema hayo Jumatano wiki hii alipotembelea katika Jumba la Makumbusho ya Kijeshi la Mapinduzi ya Umma ya China.

Xi alitembelea maonyesho ya mafanikio yaliyopatikana katika kuimarisha ulinzi wa nchi na majeshi katika zama mpya.

Xi alisema, tangu ulipofanywa Mkutano Mkuu wa 18 wa CPC Mwaka 2012, Kamati Kuu ya CPC na CMC zimekuwa zikiongoza vikosi vya kijeshi katika kuimarisha jeshi kisiasa, kuongeza nguvu ya kijeshi kupitia mageuzi na teknolojia, na kuongeza uwezo wa jeshi kwa kutegemea vipaji , kusimamia jeshi kwa mujibu wa sheria, na kuimarisha mazoezi ya kijeshi kwa ajili ya utayari wa kufanya mapambano.

“Mafanikio ya kihistoria na makubwa yamepatikana katika suala hili,” Xi alisema.

Akiweka bayana kuwa PLA itaadhimisha miaka 100 tangu kuanzishwa kwake katika kipindi cha miaka mitano ijayo, Xi ametoa wito wa kuwepo kwa maendeleo mapya katika kujenga vikosi vya kijeshi vyenye nguvu zaidi ili kuhimiza ustawishaji mkubwa wa Taifa la China. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha