Sanaa muhimu ya kwanza ya uchongaji mizizi ya mti ya China-“kuzuia pepo wabaya”

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 29, 2022

Katika Jumba la Makumbusho la Mji wa Jingzhou,Mkoani Hubei, kuna sanaa ya uchongaji kinyago cha mizizi ya mti “kuzuia pepo wabaya iliyogunguliwa nchini China hadi sasa ". Iligunduliwa katika kaburi la No.1 wakati wa Himaya ya Chu ya Mashan kipindi cha vita.Urefu wake ni sentimita 69.5, na urefu wa juu ni sentimita 40.5. Kichwa cha sanaa hiyo kinaonekana kama kichwa cha simbamarara, mwili wake ni kama joka, kwa jumla inaonekana kama mjusi. Kila mguu wake umechongwa kwa mfano wa nyoka, mjusi, ndege na wadudu cicada, yaani inamaanisha kuwa mnyororo wa kibiolojia wa nyoka akila mjusi, mjusi akila ndege na, ndege akila wadudu cicada. Tunaweza kuhisi thamani ya ikolojia wakati watu wa kale walipochonga sanaa hiyo ya kinyago chai mizizi. Sanaa hiyo inasifiwa kuwa sanaa muhimu ya kwanza ya sanaa ya kinyago cha mizizi ya mti ya China, na pia ni mfano wa nembo ya Chama cha sasa hivi cha Uchongaji Mizizi cha China.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha