Tanzania itajenga vyuo 3 vya elimu ya ufundi wa kazi kwa walemavu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 04, 2022

Mamlaka ya Tanzania ilisema Jumatano imeanza maandalizi ya ujenzi wa vyuo vitatu vya elimu ya ufundi wa kazi kwa walemavu.

Waziri wa taifa wa Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia mambo ya wafanyakazi, vijana, ajira na walemavu, Bw. Joyce Ndalichako alisema kuwa ujenzi wa vyuo hivyo vitatu utafanyika katika kipindi cha mwaka wa fedha 2022/2023 kuanzia Julai 1, 2022 hadi Juni 30, 2023.

Alisema kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika Mji wa Kigoma wa kando za Ziwa Tanganyika kuwa ujenzi wa vyuo hivyo vitatu vya elimu ya ufundi wa kazi utafanywa sambamba na ukarabati wa vyuo vinne vya zamani vya elimu ya ufundi wa kazi kwa ajili ya walemavu.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha