

Lugha Nyingine
China na Cambodia zaahidi kuenzi urafiki wa jadi
Mfalme wa Cambodia Norodom Sihamoni (wa pili kulia) akikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi aliyefanya ziara katika nchi hiyo huko Phnom Penh, Cambodia, Agosti 3, 2022. (Xinhua/Wu Changwei)
China na Cambodia Jumatano ziliahidiana kuwa, zitaenzi urafiki wa jadi na kufanya juhudi za kujenga jumuiya ya China na Cambodia yenye mustakabali wa pamoja.
Mfalme wa Cambodia Norodom Sihamoni alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi aliyewasili nchi hiyo, alishukuru serikali ya China na watu wake kwa msaada wao wenye thamani katika maendeleo ya jamii na uchumi wa Cambodia pamoja na mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya korona ya nchi hiyo.
Mfalme huyu alisema, uhusiano kati ya Cambodia na China umefikia kiwango cha juu zaidi ya kihistoria. Chini ya mfumo wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, nchi hizo mbili zinafanya juhudi za kujenga jumuiya ya China na Cambodia yenye mustakabali wa pamoja, na kuyafanya mashirikiano kati yao kwa kina zaidi. Hatua hizi zitaleta maslahi halisi kwa watu wa nchi hizo mbili.
Alisema, upande wa Cambodia unaunga mkono kwa nguvu zote Pendekezo la Maendeleo ya Dunia na Pendekezo la Usalama wa Dunia yaliyotolewa na upande wa China, na pia utaendelea kushikilia sera ya China moja duniani, na kusimama kithabiti kwenye upande wa China.
Wang Yi alisema, katika zaidi ya nusu karne iliyopita, China na Cambodia siku zote zinaheshimiana, kuaminiana, kutendeana kwa usawa, kufanya ushirikiano wa kunufaishana, hali hii imeweka mfano wa kuigwa kwa mahusiano kati ya nchi na nchi.
Alisema, siyo tu urafiki kati ya China na Cambodia umeleta maslahi halisi kwa watu wa nchi hizo mbili, bali pia umekuwa mali yenye thamani zaidi kwa kila upande kati yao, na pia umetoa mchango kwa amani na utulivu wa kimataifa na kikanda.
Alisifu Cambodia kwa kushikilia sera ya China moja, na alisisitiza kuwa kitendo chochote na maneno yoyote yanayokwenda kinyume cha kanuni ya China moja ni changamoto dhidi ya makubaliano ya pamoja ya dunia.
Pia aliahidi kuwa, China itaendelea kutoa uungaji mkono na msaada kadri iwezavyo kwa maendeleo ya jamii na uchumi ya Cambodia kutokana na mahitaji ya Cambodia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma