

Lugha Nyingine
Umoja wa Mataifa wasikitishwa na maamuzi ya DRC ya kumtaka msemaji wa kikosi cha kulinda Amani aondoke
(CRI Online) Agosti 05, 2022
Msemaji mkuu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres, Bw. Stephane Dujarric jana alieleza masikitiko yake kuhusu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kumtaka msemaji wa MONUSCO kuondoka nchini humo.
Dujarric amesema, msemaji huyu ambaye amethibitishwa na MONUSCO kuwa ni Mathias Gillman, alikuwa likizo na hakuwepo nchini humo.
Amesema hali imekuwa ya wasiwasi na Umoja wa Mataifa inafanya uchunguzi kuhusu kilichotokea Jumapili iliyopita, ambapo raia kadhaa wameuawa.
Ameongeza kuwa, umoja huo umewasiliana na serikali ya DRC na jamii za wenyeji ili kuhakikisha kuwa na mazungumao ya wazi.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma