Aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Kenya alaani ziara haramu ya Pelosi kisiwani Taiwan

(CRI Online) Agosti 05, 2022

Mkurugenzi mtendaji wa Chama cha Azimio la Umoja “One Kenya Coalition” ambaye alikuwa waziri wa mambo ya nje Raphael Tuju ametoa taarifa akilaani ziara haramu ya Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani Nancy Pelosi kisiwani Taiwan, China.

Tuju alisema ziara hiyo ya Pelosi ni hatua uovu ya kuchochea watu wa China ambayo inakasirisha watu na kupaswa kulaumiwa. Amesema Pelosi anashika wadhifa wa juu wa uongozi, hivyo hapaswi kuwa mtu asiyejali lolote na kutowajibika, anajua vya kutosha kuwa wajibu wa kutuliza hali ya dunia ni muhimu kuliko kuibembeleza Taiwan. Tuju ameeleza masikitiko yake makubwa na hatua yake hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha